NEW

6/recent/ticker-posts

Advertisement

BARUA YA UTETEZI KUTOKA GAZETI LA RAIA MWEMA

5 Agosti 2021

Kumb. RA/BD/V013/2021
Mkurugenzi,
Idara ya Huduma za Habari – MAELEZO,
Mji wa Serikali Mtumba, Mtaa wa Habari,
S.L.P. 25, DODOMA. 

YAH: UTETEZI

Rejea barua yako ya tarehe 3 Septemba 2021, yenye Kumb. Na. IH/PML/52, iliyotutaka kujieleza kutokana na habari iliyoandikwa na gazeti la Raia Mwema, toleo Na. 853, ambayo imebeba kichwa cha maneno kisemacho: "Hamza wa CCM hatari."

Kwenye barua hiyo, umeeleza kuwa habari tuliyochapisha ina upungufu wa kisheria wa taaluma kwa kuwa tulitaka kuuaminisha umma, kwamba Hamza ambaye Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura, amemtaja kuwa ni gaidi wa kujitoa mhanga na mfia dini, ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), "bila kuwa na uthibitisho usioacha shaka."

Kwamba, hatua hiyo imelenga kuleta chuki miongoni mwa wanachama wa chama hicho, na kwamba msingi wa barua yako kwetu, ni malalamiko uliyopokea kutoka CCM.

Maelezo ya Utetezi:

Kwanza, mpaka sasa, hatujapokea malalamiko yoyote kutoka chama hicho, kuhusiana na habari tuliyochapisha.

Na kwa kuzingatia uhusiano mzuri wa kikazi kati yetu na CCM, pamoja na vyama vingine, kama wangewasiliana na sisi moja kwa moja, tungeweza kujadiliana na hatimaye tungechapisha ufafanuzi wao, kwa sababu gazeti hili, halikuwa na nia mbaya wala dhamira ovu katika kuandika habari hiyo.

kujadiliana na hatimaye tungechapisha ufafanuzi wao, kwa sababu gazeti hili, halikuwa na nia mbaya wala dhamira ovu katika kuandika habari hiyo.

Aidha, hata katika barua yako kwetu, hukuambatanisha barua iliyotoka CCM, ili kutusaidia kufahamu kwa mapana msingi wa malalamiko yao na kujibu kwa ufasaha kile kilicholalamikiwa.

Pili, gazeti linalodaiwa kulalamikiwa na chama hicho, halijaandika mahali kokote katika habari yake, kwamba kinahusika na ugaidi wa Hamza. Badala yake, gazeti limemtaja "Hamza wa CCM" kama utambulisho na siyo kwamba alikuwa anakitumia kufanya ugaidi.

Tatu, kuhusu madai kuwa tumemwelezea Hamza kama mwanachama wa CCM bila kuwa na uthibitisho, napenda kukuhakikishia kuwa hakuna kokote ambako gazeti limesema Hamza, ni mwanachama wa chama hicho.

Gazeti limemtaja Hamza kuwa ni kada wa CCM, na kwamba kuwa kada wa chama, sio lazima uwe mwanachama.

Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili ya Oxford, "kada ni mfuasi wa chama fulani aliyeandaliwa kutetea siasa ya chama chake."

Kule kuvaa sare za chama husika na kujihusisha na shughuli zake, kukifadhili na kukipigania; kunamtosha kuitwa kada, hata kama hakuwa mwanachama.

Hamza alikuwa akivaa sare za chama hicho. Alikipigania kwa kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Lupa, Mashache Kasaka na amekifadhili kwa kukijengea ofisi, katika tawi la Kitete, kata ya Bwawani, wilayani Chunya.

Kama hiyo haitoshi, Raia Mwema halikuwa la kwanza kumuita Hamza kada wa CCM. Baadhi ya vyombo vya habari, vikiwamo televisheni na Online TV, viliripoti mahojiano na baadhi ya viongozi wa chama hicho wilayani Chunya wakisikitishwa na tukio hilo, na kumtambulisha kuwa alikuwa "mwenzao kwenye chama."

Naye Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, katika moja ya mikutano yake na vyombo vya habari, alimtaja Hamza kama kada wa CCM na kutumia nafasi hiyo kukipa pole chama hicho.

Kwa muda wote huo, hakuna kokote ambako CCM kimetoka hadharani kumlalamikia mwenyekiti huyo wa NCCR- Mageuzi na vyombo hivyo, hadi Raia Mwema lilipoandika habari hiyo, Sisi tunajiuliza, "KULIKONI?"

Katika habari hiyo, DCI Wambura alisema, Hamza alikuwa amejificha kwenye kichaka cha jamii kufanya ugaidi, nasi tulitaka kuionesha jamii, kwamba alikuwa amejificha kwenye kichaka cha ukada wa chama tawala, wakati ni gaidi.

Raia Mwema kama chombo cha habari, kililenga kulaani na kuvitaka vyama viwe makini na baadhi ya wanachama na makada wanaowapokea.

Tunasisitiza, kwamba hatukuwa na dhamira mbaya, lakini kama CCM wanaona tumewakwaza kwa bahati mbaya kuandika habari hiyo, tuko tayari kuchapisha ufafanuzi wao.

Kutokana na muktadha huo, tunapenda kuifahamisha ofisi yako kuwa gazeti halikuwa na nia ovu bali kuelezea kilichosemwa na DCI na hasa kutokana na hamu na shauku ya wananchi kutaka kujua zaidi taarifa za Hamza.

Tunaweka hapa ushahidi kama ulivyoelekeza, kuthibitisha ukada wa Hamza, uliotajwa kwenye gazeti. 

  • Picha za mnato zinazomuonesha Hamza akiwa amevalia sare za CCM, pamoja na zile anazoonekana akimnadi mgombea ubunge wa chama hicho, katika jimbo la Lupa, Mashache Kasaka, huko Kitete (kiambatanisho Na 1).
  • Picha za Hamza akiwa amevaa sare za CCM (kiambatanisho Na 2). 
  • Kauli za viongozi kadhaa, akiwamo Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji cha Kitete (CCM), Kata ya Bwawani, wilayani Chunya, Erick Mwashiuya na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UV-CCM), tawi la Kitete, William Heneriko, wanaothibitisha kuwa Hamza alikuwa kada ndani ya chama chao na "aliipenda CCM ndani ya moyo wake-" Mwananchi Digital (kiambatanisho Na 3).
  • Kauli za viongozi kadhaa wa CCM katika Kata ya Bwawani, wakithibitisha ukada na uanachama wa Hamza ndani ya chama chao - Azam TV, kupitia taarifa ya habari ya tarehe 27 Agosti 2021 (kiambatanisho Na 4).
  • Kauli ya mwenyekiti wa CCM, tawi la Kitete, zinazoonyesha kuwa Hamza alifadhili ujenzi wa ofisi ya tawi hilo - Ayo TV (kiambatanisho Na 5).
  • Kauli ya Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia alipozungumza na waandishi wa habari, ambapo alimtaja Hamza kama kada wa CCM - Mwanahalisi TV (kiambatanisho Na 6).
  • Kauli ya William Heneriko, rafiki wa karibu wa Hamza na Mwenyekiti wa UV-CCM, huko Kitete, akithibitisha kuwa Hamza alikuwa kada wa chama hicho na mfadhili wake.
Alifahamika kwa viongozi mbalimbali wilayani Chunya na mkoa wa Mbeya. (kiambatanisho Na 7).

Utetezi wa DC:

Kuhusu kichwa kisemacho, "DC kizimbani akidaiwa milioni 100," tunasita kukubaliana na maudhui ya barua yako, kuwa tulikiuka maadili ya uandishi wa habari, kwamba kichwa kinaonesha DC yuko madarakani.

Kwa mujibu wa uandishi wa habari, kichwa cha habari hakiwezi kubeba maneno yote, na badala yake hufupishwa na maelezo kuonekana kwenye habari yenyewe.

Ndivyo ilivyokuwa katika aya ya kwanza ambayo ilisomeka: "Mkuu wa Wilaya ya Tabora wa zamani...".

Aidha, umekuwa utamaduni wa kawaida wa vyombo vya habari kutumia vyeo vya wastaafu kwenye uandishi wetu.

Kwa mfano, Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, unaweza kuandika, "Rais Kikwete atoa msaada," na usibadilishe maana; au mtu ambaye amewahi kuwa mbunge, mpaka leo, bado jamii inamuita mheshimiwa na vyombo vya habari, vinaweza kumtambulisha kama mbunge kwenye kichwa chake cha habari, kama ambavyo sisi tumefanya, lakini ndani, kuanzia para ya kwanza, tumeandika Mkuu wa wilaya mstaafu.

Tunatanguliza shukrani.

Joseph Kulangwa,
KNY: Mhariri Mtendaji.






Post a Comment

0 Comments