NEW

6/recent/ticker-posts

Advertisement

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KIMEENDELEA NA MISIMAMO YAKE JUU YA KAULI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NA POLISI KUZUIA MIKUTANO YA NDANI NA ILE YA NJE




"Siku kama ya leo miaka 4 iliyopita Makamu mwenyekiti wa Chama chetu upande wa Tanzania Bara Mhe. @TunduALissu alishambuliwa kwa risasi akiwa kwenye makazi yake Dodoma. Tunaazimisha miujiza ya mwenyezi Mungu kwa kumponya mwanadamu kwa risasi zaidi ya 16 zilizoingia mwilini" John Mrema 

"Miaka minne Jeshi la Polisi halijaweza kutoa taarifa ya uchunguzi nani alimshambulia Mhe. @TunduALissu na hawajawahi kumshikilia mtu yeyote, wanasingizia wameshindwa kufanya uchunguzi kwasabau Lissu hatoi ushirikiano. Ni juzi tu tulishuhudia tukio la Bw. Hamza akiwa anapambana na Polisi akauwawa kwa risasi lakini ndani ya siku 4 Polisi waliweza kufanua uchunguzi." John Mrema 

"Nawapa pole Waandishi wa Habari kwa Serikali kuendelea kufungia Vyombo vya Habari, tumeona Magazeti mawili yakifungiwa. Wakati Rais akihojiwa na shirika la habari la Uingereza la BBC alisema Nchi ina uhuru wa kujieleza hamna waandishi mnaolalamika." Mhe. John Mrema 

"Natoa rai kwenu Waandishi wa Habari badala ya kukaa kimya endeleeni kuandika kuhusu Sheria kandamizi kwa sababu Bw. @MsigwaGerson ametumia Sheria ya huduma ya habari kufungia Magazeti hayo." Mhe. John Mrema 

"Kama ile sheria itaendelea kuwepo hata Rais akisema kuna uhuru wa habari, hata aende akarekodi filamu hakuna mwekezaji ambaye yupo tayari kuwekeza kwenye Nchi ambayo haifuati Sheria au Sheria zake ni kandamizi." Mhe. John Mrema 

"Msajili wa Vyama vya Siasa ametoa kauli tusitishe mikutano yetu ya ndani na makongamano mpaka tutakapofanya kikao na IGP, tunatumia nafasi hii kumkumbusha Msajili ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu kuwa hana mamlaka ya kisheria kusimamisha shughuli za Vyama vya Siasa" Mhe John Mrema 

"Tunamkumbusha Msajili badala ya kusimamisha shughuli za Vyama ambavyo vinafanyika kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Nchi anapaswa amuonye na amkanye Mkuu wa Jeshi la Polisi aache kuingilia shughuli halali za Vyama vya Siasa." Mhe. John Mrema 

"Msajili kwa kauli yake anaendelea kuvunja Sheria na Katiba ya Nchi. Mosi, kitendo cha Polisi kuendelea kuvamia shughuli za Vyama vya Siasa wanatekeleza maagizo na kauli za Rais aliposema suala la Katiba Mpya, mikutano ya hadhara isubiri, sasa anahangaika na uchumi." John Mrema 

...ni mwendelezo wa kutii amri ambayo siyo halali. Juzi tu kule mkoa wa Mara RPC alisema anazuia kongamano la kudai Katiba Mpya kwa sababu sasa ni wakati wa kujenga uchumi." Mhe. John Mrema 

"Tunamkumbusha Msajili wa Vyama vya Siasa kwamba tunatimiza wajibu wetu kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 26 (1) inayosema 'Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba na Sheria za JMT'. Msajili wa Vyama pia ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba na Sheria ya Vyama vya Siasa" John Mrema 

"Hawezi akazuia shughuli za Vyama mpaka tukutane na Polisi. Pili, Msajili anapaswa afahamu Katiba ibara ya 147 (3) (4) imepiga marufuku kwa Majeshi yote kujihusisha na Vyama vya Siasa, inasema; 147 (3) itakuwa ni marufu kwa Mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa isipokuwa atakuwa na haki ya kupiga kura iliyojatwa katika ibara ya 5 ya Katiba. Ibara ya 147 (4) inasema, Kwa madhumuni ya Ibara hii Mwanajeshi maana yake ni Askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu katika Jeshi la Ulinzi, Polisi, Magereza au JKT." John Mrema 

"Msajili anaposema tusitishe shughuli za Vyama mpaka tukutane na Mkuu wa Jeshi la Polisi moja kwa moja anavunja Katiba ibara ya 147 kifungu cha 3 na 4. Sisi hatupo tayari kutii ushauri wake kwa sababu hatupo tayari kuvunja Katiba na Sheria za Nchi yetu." John Mrema 

"Msajili anafahamu ibara ya 151 (2) (C) kinasema iwapo kwa masharti ya Katiba hii kuna jambo lolote linatakiwa litekelezwe  au lishughulikiwe na Chama chochote cha Siasa basi jambo hilo litatekelezwa na litashughulikiwa na Chama hicho kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na chama kwaajili hiyo na pia kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kwaajili hiyo. Sisi Chadema tutaendelea na vikao vyetu, tutaendelea na utaratibu wetu tuliojiwekea kwasababu tunatimiza takwa la Kikatiba." John Mrema 

"Makongamano yanayoratibiwa na Baraza la Vijana (@bavicha_taifa ) kuhusu #KatibaMpya yataendelea bila kujali tumekutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi kama anavyosema Msajili na vikao vyetu vya ndani vitaendelea." Mhe. John Mrema 

"Jeshi la Polisi wakiona ni busara kuendelea kuvunja Katiba na Sheria za Nchi kuzuia mikutano yetu halali, waendelee kufanya hivyo lakini sisi hatutaacha kufanya kazi kwa sababu tunafanya kwa mujibu wa Katiba ibara ya 151 (2) (C)." Mhe. John Mrema

Post a Comment

0 Comments