NEW

6/recent/ticker-posts

Advertisement

MCHEZAJI WA ZAMANI WA PSG JEAN PIERRE ADAMS, AFARIKI BAADA YA KUWA KATIKA KOMA KWA MIAKA 39


Mchezaji wa zamani wa ufaransa Jean Pierre Adams , ambaye alikuwa katika koma kwa miaka 39 amefariki akiwa na umri 73. 

Adams alikuwa amelazwa hospitalini kufanyiwa upasuaji wa goti lakemwezi machi 1982 lakini hakupata tena ufahamubaada ya makosa ya daktari aliyemdunga sindano ya kulaÅ‚a. 

Akiwa mzaliwa wa Senegal , beki huyo alishiriki zaidi ya mechi a140 akiicheze klabu ya Nicena pia aliichezea klabu ya Paris St- Germain. 

Katika Taarifa, PSG ilisema kwamba mchezo wa mchezaji huyo unafaa kuheshimiwa. 

Nice ilisema kwamba itamuomboleza Adams – ambaye aliichezea Ufaransa mechi 22kati ya mwaka 1972 -1976 kabla mechi iliotarajiwa dhidi ya Monaco Novemba 19. 

Adams pia aliichezea klabu ya Nimes 84 , ambayo ilisema kwamba inatuma risala za rambirambikwa familia ya mchezaji huyo. 

Siku ambayo Adams alifanyiwa upasuaji baada ya kupata jereha la goti lake – ambalo alipata wakati alipokuwa katika mazoezi – ambapo wafanyakazi wengi wa hospitali katika klabu jiyo walikuwa katika mgomo. 

Upasuaji wake ulifanyikahuku daktari anayehusika na kudunga sindano ya ganzi akihudumia wagonjwa wengine watu wanane, ikiwemo Adams wakati huo mmoja. 

Adams alisimamiwa na daktari aliyekuwa akijifunza , ambaye baadaye alisema: Sikuweza kazi niliopatiwa. Kati ya daktari huyo na mwanafunzi wake , makosa kadhaa yalifanyika , na kumfanya Adams kupata mshtuko wa moyo na kuharibika ubongo. 

Ni hadi katikati ya mwaka 1990 ndiposa daktari wa sindano za ganzi na mwanafunzi wake waliadhibiwa – wakisimamishwa kazi kwa mwezi mmoja na kupigwa faini 

Ya Yuro 750 . 

Adams alitolewa katika hospitali hiyo baada ya miezi 15 na alikuwa akiangaliwa nyumbani Nimes na mkewe , Bernadettetangu wakati huo.

Post a Comment

0 Comments