TIBA YA
MAGONJWA SUGU
KWA KUTUMIA
VYAKULA VYA ASILI
JIFUNZE JINSI YA KUZUIA NA KUTIBU
SARATANI KWA VYAKULA
Jitibu vidonda vya tumbo (ulcers), Uvimbe wa tezi ya shingo (Goiter) na magonjwa mengine sugu kwa kutumia vyakula.
UTANGULIZI
Mabadiliko yaliyokuja na maendeleo katika ulimwengu wa sasa, yamefanya wanadamu kuachana na utaratibu wa maisha ya kikale na kukumbatia aina ya maisha ambayo yanasababisha madhara kwa afya.Hii inatokana na kupuuza utaratibu wa maisha unaolinda mwili wa mwadamu na kuusaidia kujikinga na Magonjwa mbalimbali kupitia vyakula na mazoezi. Hali hii imefanya mwanadamu ajikute amekkuw mhanga wa matatizo mengi ya kiafya ambayo yangeweza kuzuilika kwa njia rahisi tu endapo angefuata utaratibu fulani wa maisha.
Uchafuzi wa mazingira, ulaji wa vyakula visivyo vya asili na sitalehe fulani fulani zilizokuja na utamaduni wa kisasa, ni vitu vilivyomfanya awe jalala la ainazote za taka na sumu ambazo zinamuingia kwa nija ya hewa,mionzi,chakula na hata vile vitu anavyo kunywa. Hii imeufanya mwili kuelemewa na mzigo wa sumu ambazo mda wowote ziweza kuwa chanzo cha ugonjwa wowote. Hata hivyo habari njema nikuwa vyakula fulani vya kila siku,mazoezi,pamoja na maji masafi, ni vitu vinavyoweza kumsaidia mwadamu kuusafisha mwili, kuutibu na kuukinga dhidi ya matatizo mengi ya kifaya yanayoonekana kumuelemea mwadamu.
VIDONDA VYA TUMBO
Miongoni mwa magonjwa yanayoshika kasi katika taifa la.Tanzania ni vidonda vya tumbo ambavyo kwa kiasi kikubwa hutokana na mifumo mibaya ya maisha ya mwanadamu na kutozingatia aina ya vyakula sahihi kwaajili ya kulinda afya.
Ugonjwa huu huibuka baada ya kutokea vidonda kwenye kuta za utumbo wa mwanadamu ambavyo hutokana na kuzidi kwa kiwango cha tindi kali yenye kazi ya kuyeyusha chakula kiingicho mwilini.
Endapo mgonjwa hatapatiwa tiba mapema tatizo linaweza kuwa kubwa zaidi kufikia kwenye mishipa ya damu hivyo hali kuwa mbaya zaidi. Yapo mambob mengi yanayo sababisha uwepo wa tatizo hili nayo ni amoja na; msongo wa mawazo, aina ya vyakula na mifumo ya maisha. Lakini watalamu wa masuala ya afya wanaeleza kuwa chanzokikubwa cha tatizo hili ni bakteria anayejulikana kwa jina la “Helicobacter pylori” ambaye bado hajapatiw suluhisho la kitabibu.
CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO
Kwa kawaida tumbo la mwadamu linatabia ya kujikinga na matatizo mbalimbali ya kiafya vikiwemo vidonda vya tumbo. hukinga tatizo hili kwa kuzalisha ‘ute’ambao hufanya kazi kama kinga ya kuzuia tindikali aina ya haidrokloriki na kimeng’enyo cha ina ya pepsin kutoleta madhara mwilini. Ikiwa uzalishaji huu hautafanikiwa ndipo vidonda vya tumbo hutokea.
Lakini sababu ya msingi kwa tatizo hili kutokea ni bacteria ‘Helicobacter pylori’ ambao wanauwezo wa kuishi kwenye ukuta wa tumbo wakiwa chini ya ute unaofanya kazi kama kinga dhidi ya athari za tindikali
Udhaifu wa mwili wa mwili katika kuzalisha ute unaotumika kujikinga na madhara ya tindikali wakati wa kusaga chakula tumboni. Matumizi ya kahawa kwa wingi husababisha uzalishaji wa tindikali kwa kiasi kikubwa.
KUMBUKA
Matumizi ya pombe hayajathibishwa moja kwa moja kuchangia upatikanaji wa vidonda vya tumbo lakini ukweli ni kwamba kilevi huchelewesha hatua za uponaji wa tatizo hili.
Msongo wa mawazo hautajwi kusababishwa ugonjwa wa vidonda vya tumbo lakini unaongeza maumivu ya vidonda kwa mgonjwa hivyo ni vyema kuepukana na halopia.
DALILI ZA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO
Kunaweza kusiwe na dalili za moja kwa moja za ugonjwa wa vidonda vya tumbo lakini malanyingi ishara zifuatazo zimekuwa zikijitokeza hivyo ni vema kumuona mtaalam wa masuala ya afya kwa ajili ya ushauri za kitabibu ikiwa ni pamoja na kufanyiwa vipimo ili kubain tatizo
-Maumivu makali ya tumbo kwa mda mrefu hususan nyakati ambazo mhusika wa tatizo hajapata chakula
-Kutapika mara kwa mara
-Kukosa hamu ya kula
-Kupungua kwa uzito
-Mwili kukosa nguvu
-Tumbo kujaa gesi
-Kutapika damu
MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO
ama yalivyo magonjwa mengine, vidonda vya tumbo vina madhara endapo havitapatiwa tiba ya uhakika au endapo mhusika atashindwa kufuata maelekezo aliyopewa na dakitari kwa ukamilifu wake.
Miongoni mwa madhara yake nia kama ifuatavyo:
a) Wakati mwingine husabaisha kufanyika kwa upasuaji mkubwa tumboni ili kuondoa eneo lote lililoathilika
b) Kupungua kwa uwezo wa kufanya tendo la ndoa na hali hii malanyingi huwakuta wanaume.
c) Uwezo wa kufanya kazi kwa ufasaha hupngua.
d) Kulika kwa utumbo hali inayoweza kupelekea kuvuja damu kwa ndani.
e) Msongo wa mawazo
JINSI YA KUBAINI VIDONDA NYA TUMBO
Wataalamu waliobobea wanaweza kuwa na suluhisho jema katika kubaini tatizo hili kupitia namna nyingi, mfano vipimo vya x-ray vinaonesha moja kwa moja maeneo yaliyo athirika hivyo kurahisisha upatikanaji wa dawa. Daktari pia anaweza kupima kiasi cha bakteria ‘H.pylori’ kwa kutumia kifaa kinachoitwa fiber-optic endoscope, ambacho kitamsaidia kubainia tatizo kabla ya kutoa ushauri wa kitabibu kipimo hiki hufanywa kwa kuingiza tumboni kifaa cha kamera chenye umbo mfano wa bomba jembamba mbacho huwezesha daktari kuona vilivyo tumboni kama inavyoonyeshwa hapo chini.
MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUEPUKANA NA TATIZO LA VIDONDA VYA TUMBO
i. Epuka matumizi ya sigara na tumbaku ili kujikinga na athari za kupata vidonda vya tumbo. Sigara na tumbaku zina kemikali inayo itwa nicotaine ambayo inaweza kusababishia vidonda vya tumbo. Tafiti zinaonyesha kuwa watumiaji wa sigara na tumbaku wanauzekano mkubwa wa kupatwa na ugonjwa huu.
ii. Kula mlo kamili kwa wakati muafaka na epuka viporo
iii. Punguza matumizi ya vyakula vyenye asili ya ges kama maharagwe, njegere n.k
iv. Matunda yenye tindikali nyingi sio mazuri hususani kwa mgonjwa aliyeanza dozi ya vidonda vya tumbo. Mfano wa matunda hayo ni machungwa, ndimu, Limao n.k
v. Epuka kuwa na msongo wa mawazo kwa wakati mwingine hupunguza uwezo wa mwili kuzuia kiwango cha tindikali mwilini.
TAHADHARI
Ø Matumizi ya dawa za kienyeji ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kina yanaweza kuwa na madhara makubwa zaidi kwa mgonjwa mwenye tatizo hili
Ø Ugonjwa huu hautokani na dhana ya kurogwa.
Ø Badili mwenwndo wa maisha kwa kuanzia katika matumizi ya vyakula mpaka vinywaji.
TIBA ZA ASILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
TIBA YA MAJI
Tiba hii inafaa kwa kutibu vidonda vya tumbo vilivyo hatua za awali.
Mgonjwa anapaswa kunywa lita moja ya maji masafi na salama alfajili kabla jua kuchomoza na kabla hajakisafisha kinywa. Kisha mgonjwa anapaswa kusubiri kwa dakika 45 mpaka saa nzima ndipo asafishe kinywa na kupata chakula cha asubuhi.
Wakati wa mchana mgonjwa anapaswa kunywa tena maji lita moja dakika 45 kabla ya kupata chakula cha mchana na asinywe maji yoyote baada ya kula chakula hicho cha mchana kwa dakika 45
Wakati wa usiku mgonjw anapaswa kunywa maji lita moja dakika 45 kabla ya kula chakula cha usiku na akae dakika45 kabla ya kwenda kulala.
Tiba hii huchukua mda wa siku kumi mpaka mwezi mmoja kabla yakupata nafuu. Katika kipindi hiki chote mgonjwa anapaswa kuzingatia mashariti juu ya ulaji na vitu vya kuepukwa yaliyoainishwa mwanzoni mwa sula hii. Kunywa juis ya kabeji mbichi baada ya kuikatakata vipande kasha isage kwenye mashine ya kutengenezea juisi(Blender).Baada hapo pima kwenye kikombe kimoja cha chai na unywe mara nne kwa siku. Tiba hii inaweza kutibu tatizo la vidonda vya tumbo kwa muda wa siku kumi. Kumbuka kuzingatia masharti ya msingi yaliyo ainishwa hapo juu.
Asali inachembechembe za asali zenye kuua bacteria na virusi ambazo vinauwezo wa kuuwa helicobacter pylory ambao ni wadudu wanaosababisha ugonjwa huu kitu kinachomaanisha kuwa ina uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo. Kingine ni asali huweza kulainisha, umio, mfuko wa chakula na utumbo hivo huweza kufunika vidonda vilivyopo tumboni. Kutokana na vidonda maumivu ya kuchoma pamoja na dalili nyingine za vidonda vya tumbo hupungua.
Asali pia huweza kuondoa uvimbe na kusafisha vidonda ambavyo hujitokeza kwenyw njia ya chakula. Asali inayopaswa kutumika kwa kusudio hili inapaswa iwe mbichi na isiwe imeongezewa vitu vingine na dozi yake ni vijiko vya chakula viwili mpaka vitatu kwa siku.
Vitunguu swaumu
Viungo hivi ni tiba nyingine inayofaa sana katika kutibu vidonda vya tumbo kutokana na kemikali zinazoua wadudu pamoja na virusi zilizomo ndani yake na hivyo huweza kupambana na kuua bacteria wanao sababisha vidonda vya tumbo.
Viungo hivi hufahamika kwa kusaidia katika kutibu vidonda vya tumbo hata pale vinapotumika vikiwa vimechanganywa na vyakula vingine kutokana na nguvu nyingi iliyomo ndani yake na chembechembe zenye kuamsha na kuboresha mwili zilizomo ndani yake ambazo huwezesha kuukinga mwili dhidi ya maambukizi kama vile vidonda vya tumbo. Hivi ndivyo unapaswa kutumia vitunguu swaumu kwaajili ya kutibu tatizo hili.
Kula punje tatu mpaka nne za kiugo hicho kwa siku zikiwa zimechanganywa na kijiko kimoja au viwili vya asali kwa siku.
Jibini Ngumu iliyosagwa (Grated cheese)
Kula jibini ngumu husaidia kufunika vidonda nya tumbo hivyo hupunguza maumivu makali ya vidonda kwa hiyo iliwe kwa wingi na mtu mwenye tatizo hili na kwawale ambao vidonda vyao vina muda mfupi tangu kujitokeza hupotea baada ya mda mrefu wa matumizi ya mara kwa mara ya chakula hiki.
Ukizingatia tiba hizi pamoja na mashariti ya kufuata ukiwa unaugua ugonjwa huu yaliyoainishwa huko mwanzoni, kunauwezekano mkubwa wa kupona tatizo hili na kuendelea kuishi maisha yenye furaha.
0 Comments