Pitch pamoja na kuwa na maana nyingi lakini katika ujenzi inatumika kama mwinuko wa paa unaotengeneza slope
PITCH IPI (mwinuko) NI SAHIHI KWA PAA ZISIZO ZA MFICHO.
Kiufundi paa linaweza kuwa ni somo maalumu kutokana na vipengele vya kuvizungumzia kuwa vingi.
Hiyo inatokana na kuwa viezekeo viko vingi na baadhi ya roof structures ni tata.Hata hivyo kila mtu anaweza kujifunza , tena kwa muda mfupi kuliko ujenzi mwingine.
Kwasababu hiyo leo nitaongelea kuhusu pitch, RUN, RISE na mapendekezo ya paa liwe na wastani wa kimo gani?
TOFAUTI YA PITCH NA PAA.
Paa ni mjumuiko wa roof structure members zote zinazotumika kuunda paa kwa ujumla wake, yaani mbao, bati nk.
Pitch ni mwinuko wa paa unaotengeneza slope.
Zingatia; kuna aina za paa na aina za miinuko ya paa (pitch) pia kuna aina za pitched roof, ni vitu vitatu tofauti hapo.
Aina hizo za pitch ni:-
1.flat roof (paa za flat) chini ya 2/12
2.low slope roof (paa za mwinuko wastani) chini ya 4/12
4.Standard and steep slope roof (paa wastani na za mwinuko mkali) zinaanzia 4/12 na kuendelea.
PAA LINAPENDEKEZWA LIWE NA SLOPE KIASI GANI.
Wastani mzuri wa mwinuko wa paa la kawaida, unapendekezwa walau uwe ni kati ya nyuzi 20° mpaka 30° .Hiyo ndiyo inayoitwa roof angle au pitch angle.Kwa lugha nyepesi mwinuko wa paa.
SLOPE YA PAA INAPATIKANAJE?
Kiufundi slope inapatikana kwa uwiano wa kupandisha 3 inch (RISE) kwa kila 12 inch ya RUN ya paa.Tazama mchoro hapo chini uone RUN na RISE.
(figure 1)
RUN NA RISE NI KITU GANI.
Run ya paa ndiyo ile nusu ya mapana ya jengo (Half ROOF SPAN ) au nusu ya eneo lolote katika mapana ya jengo linalokusudiwa kuwekwa paa.
Tazama mchoro kuona SPAN ya paa.(figure 1).
Hivyo basi, kama utatumia kanuni ya 3"/12" kupaua, inamaana utahitaji kupandisha RISE 3inch kwa kila 12inch YA RUN.
Hiyo ni kusema kama paa litakuwa na inch 12 yaan foot 1 ambayo ni Nusu ya upana wa jengo, basi slope yake au pitch yake itakuwa na Rise ya inch 3 tu.
Tazama mchoro figure 2.
KWANINI IWE INCH 3 KWA KILA FUTI 1 YA ULALO WA TOKA CENTER YA UPANA WA JENGO "RUN" ?.
Maji hayahitaji mambo mengi, yanachohitaji ni slope tu yanafuata.
Kwa sababu hiyo kama unapaua eneo lenye (Span) ya 6m ambayo nusu yake ni 1.5m sawa na RUN ya 5ft , utalazimika kupanda 15inch pekee KUPATA SLOPE YA PAA (PITCH). Zingatia kila inch 12 ya Run utapanda kwa uwiano wa inch3 (Rise).
KUNA UWEZEKANO WA KUONGEZA UWIANO KUPATA PAA LA SLOPE KALI AU KUPUNGUZA.
Hata hivyo kwa kufuata mtindo wa kisasa wa upauaji kila mtu hupendelea ratio yake.K
una sababu mbalimbali za kupunguza au kuongeza ratio ya RISE na RUN ikawa chini ya inch 3 kwa kila 12inch au ikaongezeka.
Hapo ndipo tunapata zile aina 3 za pitch yaani paa zote zenye kiwango cha;-
1.chini ya uwiano wa 2/12 ni flat roof pitch
Nitaeleza siku nyingine zinakuwaje.
2.chini ya uwiano wa 4/12 ni low slope roof pitch.
3.za juu ya uwiano wa 4/12 na kuendelea standard na steep slope roof .
PAA ZIPI ZISIZO NA KIZUIZI CHA KUINUA SANA
Hakuna sababu kubwa ya kuinua sana paa zaidi ya ile ya kuzia barafu kudumu muda mrefu juu ya paa na mvua za juu ya wastani.
Vinginevyo paa lililoinuliwa sana linaathili nyumba kwa kuzuia kani kubwa zaidi ya upepo , ambao ni mzigo kwa jengo muda wote.
Kwa hapa nchini watu wengi hupendelea paa ndefu kwakuwa zinaleta ufahari wa jengo.
Pamoja na kuwa sio lazima kuwa na paa ndefu au yenye slope kali, ila ieleweke kuwa Bati za kawaida (METAL SHEETS) hazina kizuizi cha kuinua sana au kupunguza ratio ya RISE na RUN.
Zinaweza kupauliwa kwa kuongeza ratio ya 4"/12" ambayo ni wastan wa nyuzi (18.4°degree angle) au 12"/12" ambayo ni wastani wa foot 1(RISE) kwenda juu kwa kila foot 1 (RUN) ya ulalo toka center ya upana wa jengo .
Kwa maana nyingine, huo ni wastani wa nyuzi (45° degree angle)
INAKUWAJE
Fundi au mteja anaweza kuamua kwa sababu binafsi kupandisha paa kwa jinsi anavyopenda.Fundi anaweza kupima nusu ya upana wa jengo mfano ft12 na kupandisha kiasi hichohicho cha ft12 kwa kufuata uwiano wa 12"/12" na kupata pitch ya 12/12.
Wengine huenda hata zaidi ya hapo yaani 13/12_15/12_16/12 na kuvuka mpaka nyuzi 63.4° ambayo ni ratio ya juu 24/12 .
JE NI PAA GANI HALIPASWI KUPANDISHA KUPINDUKIA.
MAPAA YA VIGAE
Hizi paa hazina uhuru wa kupandisha kupindukia
Paa la kigae linapendekezwa kutumia ratio ya 4"/12" mpaka 6"/12". Umuhimu wa kuwa na slope ya wastani kwenye paa ni kwamba maji hutiririka kwa utaratibu na kufuata mifereji.Paa likiinuka sana maji husambaa kwa kusukumana haraka na huwenda yasifuate njia yake kwa wakati.
Mfumo huo kwenye vigae haiwezi kuwa mzuri kutokana na muundo wa vigae na upauaji wake.
Zipo sababu nyingine tunaweza kuzungumza kwenye kipengele cha vigae.
JE PITCH IPI NI BORA ILI NYUMBA ISIWE NDEFU WALA FUPI.
PITCH ninayoipendekeza mimi ni ile ya angalau 12"/12" yaan 45°. Japo unaweza kuanzia kwenye ile ya 9/12.
Note.Uwiano wa ratio ndiyo unaokuongoza kupata (mwinuko) pitch ya nyumba nzima hata kama itakuwa na mapaa mengi.Ni kitu cha kawaida sana ukitembea na ratio.
Fundi michael
0 Comments