Umuhimu wa mkanda unatokana na zile nondo zinazowekwa mle ndani.
NONDO ZINA KAZI GANI KATIKA ZEGE?
Zege ina uwezo mkubwa katika kuhimili mgandamizo, lakini haina uwezo mkubwa kuhimili mvunjiko.
Hivyo zege iliyoimarishwa kwa nondo huwa imara kimvunjiko pamoja na mkandamizo.
MKANDA WA ZEGE UNA KAZI GANI?
Mkanda wa zege una kazi ya kupokea mzigo wote wa jengo, yaani ule ulio hai na uliokufa na kuutawanya kwa kiwango sawa kwenye tofali za msingi.Kwasababu hiyo msingi hubaki salama
MZIGO WA JENGO HAI NA ULIOKUFA NI NINI? (DEAD &LIVE LOAD )
Mzigo uliokufa wa jengo ni ule uzito wote unaotokana na material yaliyotumika kujengea, pamoja na vifaa vilivyofungwa kwenye jengo.Pia mzigo wa jengo ulio hai, ni ule uzito unaotokana na vitu vya mpito vinavyotua juu au kusukuma pembezoni mwa jengo.
MATERIALS ZINA UZITO GANI KATIKA JENGO. (DEAD LOAD)
Mfano paa pekee kwa nyumba yenye
Choo
Sitting
Dining
3Rooms
Jiko
Maktaba
2Veranda
PAA
Linakadiriwa kuwa na uzito usiopungua 3tonnes(tani tatu) hiyo ni mbao zinazotumika, misumari,bati nk.
TOFALI
Tofali linakadiriwa kuwa na 12kg mpaka 15kg.
Wastani wa tofali zinazojengwa juu ya msingi wa nyumba niliyoitaja, sio chini ya 2000.Ukizidisha kwa 15kg ni sawa na tonne 30.
CEMENT
wastani wa cement itakayotumika kujengea tofali juu ya msingi ni mifuko isiyopungua 35.Ukizidisha kwa 50kg ni sawa na 1.75 tonne.
ZEGE
Makadirio ya zege ya wastani wa 3M³ kwa mikanda ya zege na nguzo, yanafikia kiasi cha tonne 7.2 kila cubic meter 1 ya zege ni kiasi cha tani 2.4.
MCHANGA
Kiasi cha mchanga wa lorry 3 zenye 6m³ kila moja, ni makadirio yanayoweza kutumika kwa ujenzi pamoja na plaster.Unaweza kufikia tani zisizopungua 28.8.Hiyo ni sawa na kila cibic meter 1 =1.6tonne.
RANGI
wastani wa uzito wa rangi si kitu haba kwenye uzito wa jengo.Fikiria km ndoo 1 itakuwa na uzito wa Kg 20 je,! Ni uzito kiasi gani kwa ndoo 10 mpka 15.
CEILING BOARD
Fikiri kiasi cha ceiling board pamoja na mbao zinazoingia katika jengo.Vinaweza kuwa na uzito usiopungua tani 2.gypsum board inakadiriwa kuwa na uzito usiopungua 19kg.Kwa makadirio ya 55pcs pekee ni zaidi ya kg1000.unaweza jiuliza mbaoa uzito gani zitashikiria gypsum board.
FIXTURES
Nimeshindwa kupata neno fupi la kiswahili.Hivi ni vifaa vinvyofungwa kwenye jengo.
Feni, madirisha, wire za umeme, bomba za umeme,taa, air conditioners, mapazia, milango na fremu zake, mapambo, bomba za maji, masinki ya choo, nk.
Hivi vitu vyote huchangia kufanya jumla ya uzito wa jengo.
LIVE LOAD (mzigo hai) NI KITU GANI?
Kutokana na somo la Live load kuwa kubwa kidogo, naweza sema kwa kifupi kuwa ni uzito wa vitu vya mpito katika jengo.
Mzigo huo ni ule unaotokana na ukinzani unaosababishwa na vitu vinavyotua na kuondoka katika jengo.
Upepo, tetemeko,ndege wanaotua juu ya paa, vitu, watu wanaosimama sakafuni na darini au ghorofani , vyote ni mzigo ulio hai.
Hivyo vyote vinaweza kuchangia kwa sehemu kubwa katika uzito wa jengo.
Kila wakati jengo linaongezeka uzito wake na kupungua kwa kadiri mzigo hai unavyoongezeka na kupungua.Uzito huo ni nje ya uzito wa material zilizotumika kujengea.
MKANDA UNAZUIAJE MZIGO WA JENGO.
mkanda wa zege wenye nondo unapokea tani zote zinazoukandamiza msingi.Kwakuwa hauna tabia ya kusinyaa wala kuvunjika, hivyo mzigo utazunguka kupitia mkanda huo na kugawanywa sawa kushuka kwenye tofali za msingi.
Kazi hiyo ya mkanda hufanyika kila saa, kila dakika, kila sekunde kwa maisha yote ya nyumba.
Kwasababu hiyo uimara wa mkanda ndiyo uimara wa msingi na usalam wa tofali.
JE NAWEZA JENGA NYUMBA BILA MKANDA.
Nyumba isiyo na mkanda haina maisha marefu.Uzito wa jengo utakapotua juu ya matofali ya msingi, badala ya kugawanywa kwa uzito sawa, sehemu dhaifu zitakatika na kupisha mzigo utue ardhini.Baada ya muda crack zitajitokeza na baadaye mipasuko mikubwa.
Mara nyingi huwa nasisitiza,
Kuna nyumba za miaka 5, 10, 15, 20, 30, 50 mpaka 100.Je!Umuhimu wa mkanda unatokana na zile nondo zinazowekwa mle ndani.

Kuna nyumba za miaka 5, 10, 15, 20, 30, 50 mpaka 100.Je! unapenda kuwa na nyumba ya muda gani katika maisha yako?
Fundi michael. unapenda kuwa na nyumba ya muda gani katika maisha yako?
Fundi michael.
0 Comments