Sabuni ya unga |
Malighafi.
A. Solphonic lita 1
B. Sodium sulphate kilo 3
C. Optical brightener vijiko 10 vya chakula
D. Nausa vijiko 10 vya chakula
E. Soda ash kilo 3
F. Pafyumu kijiko 1 cha chakula
G. Rangi kijiko 1 cha chakula
Jinsi ya kutengeneza
Andaa malighafi kwa resho kama ilivyoandikwa hapo juu beseni na mwiko, kisha weka kimoja kimoja ukianza na herufi A __ G, huku ukikoroga mseto wako kwa muda wa dakika 15 halafu anika sehemu yenye hewa kivulini hadi ikauke.
Hapo sabuni yako ya unga itakuwa tayari, iweke kwenye vifungashio ipeleke sokoni.
Sabuni ya kusafisha vyoo |
Malighafi.
1. Sulphonics Acid Lita 1
2. Soda Ash nusu 1/2 kilo
3. Sless
4. Chumvi 1/2 kilo
5. Maji lita 17 1/2 _ 20
6. Rangi kijani
7. Pafyumu
8. Formalin
Jinsi ya kutengeneza
Weka maji lita 5 kisha anza kukoroga, ongeza lita 5 kisha lita 5 tena na mwisho lita 2
1. Sulphonics Acid lita 1
2. Soda ash nusu kilo
3. Sless nusu lita
4. Chumvi 1/2 kg
Hapo sijaweka rangi wala pafyumu ni vinzuri kuweka kwenye ndoo lita 10 ya sabuni utaweka rangi kijiko 1 cha chai, rangi ya kijani pafyumu aina ya ' Rose two one ' au pino vijiko 5 vya chakula na Formalin vijiko 3 vya chakula.
Formalin kwa ajili ya kuua wadudu ( bacteria ) ni vinzuri sana kuwemo kwenye sabuni ya chooni kwani ina kazi nyingi zaidi ya hiyo iliyotajwa.
JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NZITO YA KUOSHEA VYOMBO |
MAHITAJI
Sulphonic acid lita moja
Soda ash robo kilo
Sless au ungalol lita 1
Glyceline vijiko vitano vya chakula
Rangi kijiko kimoja
Chumvi gram 750
Tigma ya 3000
Pafyum laini ya matunda au harufu uipendayo
CDE mls 2000
Maji Safi lita 40.
KUTENGENEZA
Chukua Maji Lita 40 gawa Mara mbili ili upate Lita 20, kisha Lita 20 Moja tia tigna yote koroga hadi kupata uji mzito kisha well kando. Weka Sulphonic acid kwenye Chombo kisha to soda ash kisha koroga vyema Hadi kupata kitu Kama ugali HAKIKISHA unakoroga vyema kwa muda wa dakika 20 bila kupumzika.
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
Kisha ongeza Sless koroga vyema kwa dakika 10 kisha tia Maji Lita 20 ambayo hayana Tigna kisha koroga hadi ule ugali uishe wote (tumia fagio la chelewa Safi kukorogea ili kurahisisha)
Baada ya hapo tia Yale Maji yenye Tigna, koroga vyema kisha ongeza rangi na glycerine, CDE, endelea kukoroga Hadi iishe kisha mwisho tia Pafyumu na ukoroge kwa dakika 5 na acha sabuni iive, ifunike na uiache kwa masaa 24 na zaidi ndio ufungashe katika vifungashio peleka sokoni.
Vifaa vinapatikana SIDO popote pale unapoiona au ilipo nenda kaulizie vipo kila sample.
Asante sana rafiki sasa chukua hatua ya kufanya hakika utafanikiwa sana.
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
Hakimiliki©2022 Jumanne255 Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa "kushare" na usibadili kitu chochote bila ya idhini/ruhusa ya mwandishi.
0 Comments