NEW

6/recent/ticker-posts

Advertisement

Kuna Nyakati Unaweza Usilipwe Sawa na Unavyojitoa Hivyo Ondoa Matarajio ya Malipo Yako.


Kwani Umewahi Lishukuru Jua kwa Kutochoka Juu Yako


Tunaishi katika maumivu ambayo tungeweza kuyaepuka kabisa sisi wenyewe. Unapoweka matarajio tu katika maisha basi umejiweka katika mtego wa kuumizwa endapo ulichotarajia kisije kutokana na ulivyodhania. Watu wengi hufanya vitu ili waje kulipwa na hiki kimeleta ugomvi na mifarakano mingi kwa watu pale ambapo alifanya kitu basi alitegemea kulipwa sawa na alivyofanya. Si lazima ulipwe sawa na ulivyojitoa na wakati mwingine unaweza usipate hata kutambuliwa ukashuhudia isipokuwa wale ambao watakuja nyuma yako. Maisha kwa upande huu huwa ni mchungu sana kwa watu ambao wanafanya vitu kwa kutarajia kuwa watalipwa, watatambuliwa au kushukuriwa.

Asili inatufundisha namna isivyotarajia wema au fadhila kutoka kwa viumbe vyake ndo maana utaona jua linaendelea na kazi yake kila siku bila kuamka asubuhi kuwa imetokea limekataa kuwepo sababu tu watu hawashukuru kazi yake. Ila viumbe walio ndani ya asili hususani binadamu tumejiwekea taabu ya kufanya kila kitu tukiwa tunataka malipo ya kile tulichokifanya ambapo hutokea tusilipwe kutokana na kile tulichokifanya. Wengi huumia na kuona walistahili kupongezwa au kutendewa sawa na jinsi walivyojitoa mno kwa ajili ya kitu fulani.

Usije kuingia katika mtego wa kuwa unafanya kitu ili uje ufanyiwe hivyo siku za baadaye. Utaumia sana endapo hutafanyiwa sawa na juhudi zako ulizotoa. Fanya kama unafanya sehemu yako ya wema usiohitaji malipo. Ukilipwa au usipolipwa kwa yale uloyafanya yote yahesabie ni matokeo chanya kwako. Unapojiweka kufanya kitu ili uje ufanyiwe hivyo jiandae kuangushwa na matarajio hayo. Ona namna asili inavyoendelea kuhudumia watu bila kuchoka na hakuna siku ambayo imetokea asili imeghairisha kufanya kisa haijashukuriwa.

Post a Comment

0 Comments