NEW

6/recent/ticker-posts

Advertisement

Mafunzo Bora ya Maisha Huja na Gharama Zake Nyingi

Maumivu Hutufundisha Mafunzo Mengi Tunapoendelea Kuishi.


Vitu vya bure vina gharama kubwa kwenye maisha. Hata kama wewe utavipata bure basi jua kuna mtu kalipia na kuingia gharama na kwa kupata bure kuna gharama ambayo hujificha. Neno bure hushika hisia za watu wengi na huo ni mtego kwa siku za baadaye. Ni rahisi kupata watu wengi kwa kuambiwa kuwa ukinunua bidhaa fulani basi kuna bidhaa nyingine utapatiwa bure. Mtu anasahau kuwa amenunua bidhaa moja ila kwa kuwa kuna neno bure kwa kununua bidhaa fulani anafikiria kuwa kapata bure kumbe si kweli. Neno bure ni “mtego” unaposikia neno hilo kuna mtu atananaswa kwa siku za baadaye.

Mbali na hilo la bure, maisha yana mafunzo ambayo huwezi kuyapata bure isipokuwa kwa kupitia na kupata maumivu kabla ya kupata uzoefu, ujuzi au hekima. Maumivu ni sehemu ya maisha katika kukomaa na kupata mafunzo bora. Utapata maumivu katika biashara, fedha, mahusiano, elimu, uwekezaji na utavuna matokeo ya mafunzo katika kila kimoja utakachokuwa umepitia. Huenda ni hasara, gharama ambazo umezipata kwa vitu hivyo kunakupa mafunzo kwa ajili ya kukujengea maisha bora.

Watu wengi ambao wamepata hasara kupitia biashara na kupata maumivu sababu ya maamuzi mabovu huwa ni rahisi kujifunza vitu na wanaposimamia mafunzo walojifunza huja kuwa wafanyabiashara mahiri zaidi kuliko wale ambao hawajawahi kupoteza au kupitia maumivu. Mtu anapopitia maumivu akili huwa inajifunza zaidi, hisia huumizwa na hapo ndipo mafunzo makubwa ya maisha mtu huyaelewa vizuri zaidi. Ingawa si lazima mtu apitie makosa ili ajue umuhimu wa kujifunza kuna njia ya kujifunza kupitia wengine kunaweza kuepusha kutofanya makosa yale yale.

Maumivu ni mwalimu wa ndani wa maisha yetu kuwa kuna kitu tunapaswa kujifunza. Mtu anapoumia kunampa nafasi ya kutafakari dhidi ya mambo yalotokea. Maumivu yanampa mtu kuona ilivyo ngumu kutowazia maumivu hayo na ukawaza vingine. Maumivu hutuliza akili ya mtu na kuwaza yalomtokea. Hili husaidia mchakato wa mtu kujifunza, kuelewa ukweli wa maisha na endapo mtu akijifunza basi maisha bora huzaliwa. Furaha na uzuri wa maisha unaweza kuzaliwa katika matokeo ya maumivu na makosa ambayo mtu awali aliwahi kuyapitia.

Post a Comment

0 Comments