NEW

6/recent/ticker-posts

Advertisement

Maisha ni Kuwajibika Kila Siku Hadi Siku Tutakapokufa.


Kifo ni mapumziko baada ya nafasi ya kuishi kuisha. Ni mapumziko yanayofanya mwili usiendelee kufanya kazi zake, ubongo usimame, moyo ukome kudunda, seli za mwili zipoteze uwezo wa kufanya kazi. Kifo ni kuisha kwa kazi ya mwili. Kifo ni kufunga kwa kurasa za maisha ya uwajibikaji.

Wakati ambao bado kifo hakijabisha hodi basi ni mwito kwa kila mtu kuwajibika na kuishi sasa tukijua nafasi ya kuishi kwetu itafika ukomo wake. Kila siku mpya inapokuja inatukaribisha katika wajibu wa kuishi, wa kufanya kazi kama ambavyo Marcus anatuhimiza namna kila siku unapoamka na kujikuta kama una uchovu wa kutotaka kuamka basi jikumbushe kazi yako kubwa ya kuishi na kufanya vitu kama walivyo viumbe wengine wanapojitoa kwenda kuishi. Ndege kuendelea na maisha yake, wanyama mwituni kuendelea na maisha yao basi ndivyo hata maisha yetu yanahitaji uwajibikaji kila siku.

Siku tutakapokuwa tunafikia ukomo wa maisha yetu basi utahesabika namna siku ambazo mtu alikuwa hai alivyoweza kuwajibika na kufanya vitu vyake kila siku. Kila siku ni alama ambayo maisha hutuhitaji tufanye kitu maana kwa siku moja yaweza kutosha kuanza maisha na kuisha maisha. Tunaona namna wakati mwingine mama aliyetoka kujifungua na kwa bahati mbaya akapoteza kichanga. Utaona maisha namna katika dakika chache maisha yameisha. Dakika, saa au siku ni kitu kikubwa katika safari ya maisha ya kiumbe hai chochote duniani.

Wajibu wetu mkubwa ni kujitoa kwa ajili ya kuwa sehemu ya jamii inayotuzunguka. Kujitoa katika vipaji ambavyo tumepewa bila kukoma. Katika nafasi ya kujitoa kila siku ndivyo wajibu wetu wa maisha unavyozidi kuongezeka. Kuwajibika ndiko kunakofanya mtu afikie utoshelevu mkubwa wa hatua za maisha yake. Kuwajibika ni kupunguza nafasi baada ya kifo kumbukumbu ya mtu kufutika. Leo na miaka ijayo mingi itakayokuja watu ambao wanatimiza wajibu mkubwa wa kuishi kitoshelevu ndio majina hayatakuwa rahisi kusahaulika katika masimulizi ya vizazi vijavyo.


Post a Comment

0 Comments