Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) leo Ijumaa amewasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam.
Freeman Aikael Mbowe na wenzake watatu, wameaachiwa huru leo, na Mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa, Baada ya DPP Kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo, leo 4.3.2022. Hivyo, Freeman Aikaeli Mbowe |
Wakili wa Utetezi Peter Kibatala: wengine Juzi na Jana tulikuwa Ukonga na Segerea. Tulionana nao wakiwa na Bashasha kabisa, Kwamba Leo tunaendelea na Utetezi
Lakini Leo Asubuhi tumepata Taarifa Kutoka Kwa Askari Magereza Kwamba Mbowe amepata Matatizo ya Ki Afya. Kwa hiyo hatuwezi Kuendelea,
Hivyo, Tunaweza Kupanga Kuendelea Jumatatu
Jaji: Jumatatu itakuwa Tarehe ngapi
Wakili Peter Kibatala: Tarehe 07 March 2022
Kwa upande wa serikali
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Utetezi, na tumewasikia Wenzetu Maombi Waliyo Wasilisha
Sasa tusingependa Kujibu Hoja hiyo, Kwa sababu na sisi tuna Maombi Mengine, kwa hiyo Kujibu Hoja hiyo haitokuwa na Maana sana. Mheshimiwa Jaji tunaomba Moja la Kufanya Mbele ya Mahakama yako.
Na Ombi hili Mheshimiwa Jaji ni kwamba Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP) kwa niaba ya Jamhuri anaomba Kuwasilisha Taarifa ya Kutokuwa na Nia na Kuendelea na Shauri hili na Taarifa hiyo tunaitoa Chini ya Kifungu cha 91(1) kwa Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Taarifa Hii tunaiwasilisha kwa Njia ya Maandishi, Kwa Maombi hayo ya Kifungu cha 91(1) tunaomba Kuondoa Mashitaka Yote dhidi ya Washitakiwa Wote Sababu zote zipo katika Noel Prosecui ambayo tumeiwasilisha
Wakili wa Serikali Robert Kidando: anapeleka Nyaraka Mbele ya Karani wa Jaji, na Karani anampatia Jaji
Jeremiah Mtobesya: Tumesikia Taarifa ya Notes hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Wa Mashtaka, na Kwa Bahati Mbaya hatuwezi Kusema lolote zaidi ya Kusema tunaichia Mahakama, sababu Kifungu Kinatoa Maelezo Yote Kwamba Baada ya Kusema hivyo tunaichia Mahakama dhidi ya Amri zake za Mwisho
Jaji: Je umezungumza kwa niaba ya Defense Wote..?
Jeremiah Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba kila Mmoja aseme
John Malya: Mheshimiwa Jaji notes iliyotolewa inayushuka Mikono wote, pamoja na Kujiandaa kwa ajili ya Kujitetea, Mikono yetu imefungwa na hatuwezi Kusema lolote, Tulitaka sana Warudishe Gharama zetu na Mengine lakini wacha Tusubiri Maamuzi ya Mahakama
Fredrick Kihwelo: Kwa niaba ya Mshtakiwa wa tatu Tumesikia Taarifa iliyotolewa, Tunaichia Mahakama iweze Kutoa Amri
Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Na sisi tunaichia Mahakama, Sheria inajielezea wazi..
Mahakama ipo Kimya Kidogo na Jaji Bado anaandika
Freeman Aikael Mbowe na wenzake watatu, wameaachiwa huru leo, na Mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa, Baada ya DPP Kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo, leo 4.3.2022. Hivyo, Freeman Aikaeli Mbowe
0 Comments