NEW

6/recent/ticker-posts

Advertisement

Life is a mystery (maisha ni fumbo.)

Unaweza kupanga jambo fulani lakini maisha yakakupangia kinyume kabisa na mipango yako.
Ni mara ngapi tumeshuhudia waliokuwa na ndoto ya upilot kwa mfano wakiishia kufundisha au waliokuwa na ndoto ya kufundisha wakiwa maafisa mikopo kwenye mabenki?


Mfano Unamhusu Mkurugenzi Wa Brela Bwana NYAISA SIMANGO.
 
Bwana Nyaisa hakuwa ameota kama angekuwa afisa ugani hadi kuwa afisa utawala wa Benki Kuu,
Ndoto hii ilibidi ifanikiwe baada ya NYAISA kupata ajali kwenye meli ya MV Bukoba.
Wakati ule akiwa ni afisa Magereza.


Miaka 26 iliyopita Nyaisa Simango akiwa ni WARDER( asiye na cheo) wa Magereza Ukonga akiwa na S/sgt NIKO walipewa jukumu la kumsindikiza mfungwa kutoka Ukonga hadi gereza la Bukoba ili aende kusikiliza rufaa ya kesi yake.

Safari hii ilimgeuza NYAISA kuwa mwandishi, hakuwa na wazo kabisa kama kuna siku angekuja kuandika kitabu maishani mwake. Lakini yaliyomkuta katika safari yake akitoka Bukoba yalimfanya aandeke kuelezea mkasa huu.

NUKUU 

“ Nimeelezea kwa ufupi tu baadhi ya matukio niliyoyaona na kushiriki ndani na nje ya MV Bukoba wakati wa safari. Inawezekana nisingeyakumbuka matukio haya yaliyotokea katika meli kama ajali isingetokea, kwani kifo kilinifanya kuwa makini kupita kiasi wakati nikijiokoa.”

Safari yao alianza kwa treni Tarehe 17 May 1996 kutokea Dar es salaam mpaka Mwanza. 
Nyaisa akiwa amejifunga Pingu moja na mfungwa wake, alikuwa akimfungua Pingu wakati wa kula na kujisaidia pekee.


Nyaisa anasema abiria kwenye gari moshi walikuwa wanawachukulia wao kama watu wasio na utu, na baadhi walitoa rai amfungue pingu.
Lakini aliwahakikishia hatamfungua kamwe, anasema hakulala kwa zote tatu walizokuwa kwenye train.

He stayed vigilant all the time.

NYAISA na mfungwa wake waliwasili salama Mwanza alfajiri ya tarehe 20 May 1996. Kwa kuwa siku ile kulikuwa na ratiba ya meli ya Bukoba jioni, utaratibu ulikuwa ni kumpeleka mfungwa gereza la BUTIMBA Mwanza mpaka utakapowadia muda wa safari Nyaisa alifanya hivyo.


Nyaisa anadai alikuwa akimpa mfungwa wake “favor” nyingi tu lakini haziongelei. Lakini anamwelezea yule mfungwa kama mtu aliyekuwa ni msomi na upeo mzuri wa kuchanganua mambo. Safari ile ilifanikiwa kuwajengea kujaribu.

Kwa kuwa Nyaisa alikuwa amepewa muda wa wiki mbili kwa ajili ya safari ile, alikuwa amenuia mara tu baada ya kumfikisha mfungwa Bukoba atumie fursa ile kwenda kusalimia kijijini kwao Serengeti Mkoani Mara. Nyaisa akawa ameenda “custom” kukata ticketi ya Bukoba, Alikuta vurumai kubwa abiria wakigombea tickets. Kulikuwa hakuna utaratibu maarumu, maafisa TRC nao wakitumia fursa ile kuuza tickets za abiria na mizigo kwa bei ya “kuruka” ili kujipatia chochote. Hali hii haikuzuka bila sababu!

Hakika sababu ilikuwepo....
Kwa muda wa karibu wiki nzima, hakukuwa na huduma ya usafiri wa meli kati ya Mwanza na Bukoba.
Hii ni kwa sababu Meli iliyokuwa imepangiwa safari njia ile, Ilisimamishwa kwa ajili ya mandatory overhaul.
Kila meli itembeapo umbali wa Neutical miles maalumu ni lazima ichekiwe.
Sababu hii ndiyo ilisababisha meli ya MV VICTORIA iliyokuwa imepangiwa safari ile isimame.
Baada ya watu kukosa huduma ya usafiri ndipo ikaamuliwa meli ya MV BUKOBA iende kama mbadala.
Lakini MV VICTORIA ilikuwa na uwezo mara mbili zaidi ya MV BUKOBA kubeba abiria na mizigo.
Pamoja na yote MV BUKOBA ilikuwa imeundiwa hoja nyingi za kiufundi na ship surveyor wakidenish aliyekuwa ameifanyia meli ile “Inclination test” na kugundua kuwa MV BUKOBA ina tatizo la “Listing
Listing ni kuyumba kwa meli kutokana na movement ya abiria au mzigo.

Mtaalamu huyu MR. SORREN akaandika maoni kwamba meli ile iliyokuwa na uwezo wa kubeba abiria 400 na mzigo wa tani 200 ipunguze mzigo na ibebe tani 35 tu.
Wahusika wakatuma taarifa ile kwa mtengenezaji wa meli ile ambao ni Belgium Shipping Corporation.

Wabelgiji wakakataa taaifa
Wakasema watakuja wao kufanya test yao.
Tarehe 1 May 1996 wataalamu wale wakaja, MV BUKOBA ikasimamishwa kufanya kazi ili ifanyiwe test.

Test ikisimamiwa na afisa wa TRC aitwaye JOSEPH HIZA Kabla ripoti haijatoka, MV BUKOBA ikapiga ruti mbili kati ya Mwanza na Port bell Uganda, Katika ruti zote hizo Captain wa meli ile hakutoa malalamiko yoyote ya kiufundi.

Ndipo MV VICTORIA ikasimamishwa na kuibuka shida ya usafiri kati ya Mwanza-Bukoba. Ikapapangwa MV BUKOBA iende safari ile Nyaisa na mfungwa wakitakiwa kuwa abiria.
Nyaisa na abiria wengine hawakujua kama meli wanayoigombea ni walking dead, Nyaisa akatumia “mbinu za medani” kupata tiketi.

Mbinu hizi zilijumuisha kupigana viwiko na kuganyagana. Akafanikiwa kupata tiketi, akaenda kuwatembelea askari wenzake akivuta muda wa safari.

Meli ilipangiwa kuondoka saa 2 usiku, Nyaisa aliingia tena melini na mfungwa wake kibabe sana kwa jinsi umati ulivyoshonana. Wakafanikiwa kupata siti daraja la tatu, hili ni eneo la ndani usawa wa kitako cha meli.
Nyaisa anasema ilikuwa ni mara yake ya kwanza kupanda meli, pia alikuwa hajui kuogelea.

Baadaye akamuachia mwenzake mfungwa na yeye akaenda kupata kinywaji kwenye mgahawa wa melini maarufu kama BUFFET, Kule akakuta ulimwengu mwingine kabisa. Watu wakiponda anasa kwa kunywa pombe na vitimbi mbali mbali.
Watu wale walikuwa hawana habari na lolote lililokuwa likiendelea melini. Hii ndiyo ilikuwa maana halisi ya PONDA MALI KUFA KWAJA
Muda wote meli ile ilikuwa imeyumbia upande mmoja ikikata viuno.

Mara kukatokea myumbo mmoja hadi friji moja ya BUFFET ikaanguka na kumwaga vinywaji vikavunjika.

Ukafata ukimya baina ya walevi wale. Lakini hali ikatulia shamrashamra zikaanza upya kama hakuna lililotokea. Nyaisa akafanikiwa kusikia watu wawili wakiteta jambo lililomshtua!

Credit-Fornatus Buyobe

Post a Comment

0 Comments