SALAMU kwenu wanawake wote , najua mko gado kama nilivyo mimi, leo ni siku nyingine tumekutana tena kupeana ujanja wa kukimiliki chumba, wakiwemo waume zetu kwenye uwanja wa kujidai.
Malalamiko juu ya kutoto sheka kwenye chakula chenu cha usiku nimekuwa nikiyapata kutoka kwa wanawake wengi ambao ni wadau wangu wa safu hii, jambo linalonishangaza zaidi wengi wao wamekuwa wakinitonya kuwa huona aibu kuwaambia waume zao juu ya kutotosheka kwao!
Hee! Udhaifu wa aina gani! Hufahamu kuwa suala la kutosheka kwenye chakula cha usiku ni la lazima ikiwa mnataka ndoa zenu ziwe na furaha? Lakini hata kama haitokei hivyo hutakiwi kulifumbia macho hadi ligeuke kuwa ugonjwa sugu!
Kwa nini umuonee aibu? Mwambie ili ajue kuwa kuna tatizo ili ikiwezekana mshirikiane kutafuta njia za kulitatua.
Katika uchunguzi nilioufanya nimegundua kuwa asilimia kubwa ya wanawake ambao hawaridhiki walapo chakula cha usiku na waume zao ndiyo hao hujikuta wakiingia kwenye mchezo wa kuchepuka, wakati mwingine unawakuta hata wakitia aibu kwa kujidhalilisha kutembea na marafiki au watu wa karibu wa waume zao, jambo ambalo si sawa hata kidogo!
Mwanamke kamili ambaye anajiamini hatakiwi kuwa wa aina hiyo, hutakiwa kuwa muwazi pale ambapo anaona kuna mapungufu ili yarekebishike maana hata misemo yetu ya Kiswahili inatukumbusha kuwa, mwanamke imara huijenga ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe na legelege huibomoa.
Nikirudi kwenye tatizo hilo, wakati mwingine hutokea kwa wanawake wengi ambao chanzo huwa wao wenyewe, hawafahamu kujiachia mbele ya waume zao wawapo kwenye uwanja wa kujidai badala yake wanasubiri tu kufanyiwa kila kitu, sasa usiposhiba unataka umlalamikie nani?
Kumbuka hata huyo mumeo ni binadamu, ikiwa anakushika sehemu ambazo hazikufanyi hushtuke mwelekeze maeneo ambayo akiyafikia vizuri utapata burudani.
Kwa kufanya hivyo, mtaimarisha uhusiano wenu na hakuna atakayewaza kumsaliti mwenzake.
Wanawake nawashauri kutokuwa wakimya kiasi cha kusababisha kuyumba kwa ndoa zenu, kutoshibishwa kwenye chakula cha usiku ni jambo dogo sana ikiwa wote mna afya njema.
Vunja ukimya unapokuwa faragha, jiachie na kushirikiana vyema na mumeo, ukifanya hivyo nina uhakika utakuwa malkia wa chumba. Tukutane katika mada ijayo.
Mshirikishe Mwanamke Mwenzio Elimu Hii.
0 Comments