Makala hii imeandaliwa kwa lengo la kumkwamua mjasiriamli katika kutengeneza bidhaa mbalimbali za ujasiriamali itumie kujigunza kunatengeneza bila kufundishwa.
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
Kupitia program maalumu ya mafunzo kwa njia ya mtandao hasa kupitia blog ya jumanne255.com, watu wengi sana wamenufaika kupitia blog hii na wengi wamebadilisha maisha yao kwa kujiajili kupitia mafunzo wanayoyapata huku. Shuhuda nyingi ambazo zimetolewa na watu mbalimbali ni ushahidi tosha kuwa mafunzo haya yamewabadilisha sana. Mafunzo haya ambayo hutolewa kwa njia ya mtandao kwa kuwekwa kwenye blogger huwekwa kwa lugha ya kiswahili na huwafikia watu walioko maeneo mbalimbali. Mwaka 2017 moja ya mafunzo yaliyofanyika ni yale ambayo yalihusisha kujenga msingi wa mafanikio na unavyoweza kufanikiwa kifedha, mafunzo haya yalidumu kwa muda wa miezi 3. Kupitia blog hii jumanne255.com kupitia mafunzo hayo ni wengi walifanikiwa kupiga hatua na kutaka kuyapata mafunzo hayo kwa njia ya kitabu. Yaliyomo humu ni kutoka kwenye Kijitabu katika sehemu ndogo ya mafunzo yaliyotolewa. Lengo ni kukupa maarifa ili nawe uweze kufanikiwa katika kuiishi ndoto yako.
Makala hii imeandikwa na Janeth James Mgongo (Mama Irene), ikiwa ni makala ya 2 Haki zote zipo chini ya Janeth James Mgongo. Haki zote zimehifadhiwa.
Huruhusiwi kunakili, kudurufu au kutumia sehemu ya makala hii bila idhini ya mwandishi. Kufanya hivyo itakuwa ni Ukiukwaji wa haki za mwandishi, na ukiukwaji wa taratibu. Hii unaweza kupelekea mashitaka toka kwa waandaaji wa kazi hii. Mpangilio wa ndani umefanywa na Jumanne Mwita.
YALIYOMO
SEHEMU YA KWANZA
PILI
TATU
NNE
TANO
SITA
SABA
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUTENGENEZA SABUNI
SABABU YA SABUNI KUJIKATA AU KUJITENGA
VIFAA VYA USALAMA NA VITENDEA KAZI
VIFAA VYA MSINGI KATIKA UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA MAGADI NA TIBA
KIPIMIO
KAZI YA MALIGHAFI
SABUNI YA MAJI | ( kanuni ya kwanza )
Mahitaji
Malighafi.
Hatua Za Utengenezaji
- Chukua ndoo weka sulphonic acid kwenye chombo cha kukorogea koroga soda ash light kwenye maji lita moja na nusu mimina kwenye sulphonic acid koroga
- Weka sless kwenye mchanganyiko wako anza kukoroga.
- Weka maji kidogo kidogo lita 10 lita kumi zilizobakia korogea alka tu kisha mimina kwenye ndoo yenye mchanganyiko ule wa mwanzo
- Weka Cde,Ongeza Glycerine Koroga
- Weka Rangi Na Perfume
- Weka Dm Dmh /Nu-Care
- Pima Ph
- Weka Kwenye Vifungashio Na Fungasha
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
UTENGENEZAJI WA SABUNI YA
MAJI (kanuni ya pili
MALIGHAFI
Vifaa vya kutengenezea
Kuwa makini kuna baadhi ya kemikali hatari kwa afya
HATUA ZA UTENGENEZAJI WA SABUNI YA MAJI
1. Chukua ndoo au Jaba unaweka sulphonic acid Na Siles unakoroga kuelekea upande mmoja
2. Weka soda ash Na cmc koroga kuelekea upande mmoja
3. Weka Maji Lita 30 koroga kuelekea upande mmoja kwa dakika 5
4. Weka grisalini,pafyumu Na rangi koroga kuelekea upande mmoja
5. Weka DM dmh na chumvi ambayo uliiloweka kwenye Maji weka kidogo kidogo huku ukipima uzito upendao ,ukishamaliza hapo funika Sabuni yako iache ipoe povu lote lishuke ndipo uanze kupaki kwenye Vifungashio
NB: Usiache bila kufunika pafyumu yako itaruka nakuisha kabisa.
SABUNI YA MAJI (kanuni 3)
MALIGHAFI
HATUA ZA UTENGENEZAJI
SABUNI ZA MAJI (kanuni ya nne)
Malighafi
Maji liter 30 au 40
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Andaa maji lita 40 chota Lita 3 kisha weka kando.
2. Chukua sles tia ktk ndoo koroga tia chumvi kijiko kimoja kuyeyusha sless vizuri, koroga hadi upate cream Kama lotion iwe soft kabisa.
3. Chukua Sulfonic acid mimina ktk ndoo yenye sless kisha koroga vizuri na utie maji lita moja ili kulainisha mchanganyiko huo kisha koroga, ongeza soda ash ambayo uliiloweka ktk maji robo lita itie humo ktk mchanganyiko huo koroga vizuri ikianza kuleta ugumu anza kutia maji nusu Lita kisha koroga upate cream soft kabisa
4. Baada ya kupata cream soft endelea kutia maji lita moja moja hadi yaishe huku ukikoroga kuelekea upande mmoja pia maji tia upande katika ndoo na sio kumwagia katikati ya ndoo, ongeza chumvi kilo 1½ ile uliyoloweka koroga vizuri kabisa ilete uzito dakika 20
5. Baada ya kutia chumvi na kukoroga vizuri saana ( ukorogaji mzuri wa muda mrefu hufanya sabuni iwe nzuri na isiwe na wingu) ongeza cdea koroga.
6. Chukua alka 2/ cmc tia katika maji Lita 3 uliyotenga koroga vizuri upate uji mzito kisha miminia katika sabuni yako koroga vizuri kwa dakika 20 upate uzito zaidi ( usiloweke tigna na kuiacha itaganda na kuharibika.)
7. Tia gryceline kisha koroga,tia rangi kiasi ukitazama isizidi na kukolea saana, iwe rangi kiasi ili kuleta mvuto pia utakoroga kuelekea upande mmoja ili kuepusha povu kukuzuia kuona ndani, hii. ( Loweka rangi katika maji kiduchu ikoroge ndipo uitumie)
8. Tia ethanol 50ml na DM DMH Koroga vizuri Funika sabuni yako iache kwa iive kisha utaitia pafyum yako na kuifungasha tayari kwa matumizi.
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA MAJI
(kanuni 5)
MALIGHAFI
MAANDALIZI
1. Chukua caustic soda 60gm loweka katika maji ya 1000ml.
2. Chukua soda ash 125gm loweka kwenye maji ya 1000mls.
3. Chukua Foaming booster 80gm loweka kwenye maji ya 1000mls
NB: Viache kwa muda wa masaa mawili.
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chukua sless na sulphonic acid mimina kwenye jaba lako lisilo na maji kisha koroga kwa muda wa dk 5 hadi vichanganyike vizuri.
2. Chukua caustic soda uliokuwa umeiloweka katika maji 1000mls mwaga katika mchanganyiko wa awali kisha koroga kwa muda wa dk 5
3. Chukua soda ash iliokuwa imelowekwa katika maji ya 1000mls mwaga katika mchanganyiko wako kisha endelea kukoroga kwa muda wa dk 3 hadi 5
4. Chukua booster iliokuwa imelowekwa kwenye maji ya 1000mls mwaga katika mchanganyiko wako wa awali kisha koroga vizuri kwa muda wa dk 5
5. Chukua Tigna ichanganye kwenye maji uliyo yaandaa 22000mls sawa na lita 22 ikologe kwa dk1 ichanganyikane vizuri kisha mimina hayo maji ambayo ni mchanganyiko na Tigna katika mchanganyiko wa awali.
Kisha utaendelea kukoroga mpaka pale utakapo ona uzito.
BAADA YA SABUNI KUWA NZITO.
NOTE: Hapo sabuni yako itakuwa imekamilika kwa 90% kisha ifunike vizuri.
SIKU INAYOFUATA
NOTE: Baada ya hapo sabuni yako itakuwa tayari sasa kupeleka sokoni.
UTENGENEZAJI WA SABUNI YA MAJI MULTIPURPOSE KANUNI 5
Malighafi
JINSI YA UTENGENEZAJI
DISINFECTANT LIQUID SOAP (Sabuni ya kudekia/kusafishia nyumba/chooni.
Hii ni aina ya sabuni ambayo hutumika kusafishia au kudekia mazingira ya nyumbani. Sabunii hii huuwa vijidudu (Germs) na Bacteria wazungukao sehemu za nyumba zetu, kama vile jikoni, chooni, sebuleni na maeneo mengine. Sabuni hii ni rahisi kutumia pia ni rafiki kwa matumizi ya nyumbani. Pia huondoa madoa au uchafu sugu kwa haraka zaidi.
MAHITAJI
HATUA ZA UTENGENEZAJI
Ongeza perfume ya Lemon/Dettol au Lavender 100ml kisha koroga vizuri na acha kwa saa 24 au zaidi kisha fungasha peleka sokoni.
HAIR SHAMPOO
Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea.
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
MAHITAJI /MALIGHAFI
VIFAA
MZANI NDOO YA PLASTIKI
GLOVES MASK
BUTI MWIKO WA KUKOROGEA
HATUA ZA UTENGENEZAJI
MAMBO YA KUZINGATIA
Mfano wa vionjo
SHAMPOO YA ALOVERA NA ASALI
MAHITAJI /MALIGHAFI
VIFAA
- Mzani
- Ndoo Ya Plastiki
- Gloves Mask
- Buti
- Mwiko Wa Kukorogea
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chukua ndoo weka sless peke yake KOROGA mpaka iwe kama cream
2. Weka maji kidogo kidogo mpaka yaishe huku ukiendelea kukoroga
3. Weka CDE na glycerine KOROGA kwa dakika tatu
4. Weka alovera na asali Kisha koroga vizuri
5. Weka citric acid ,pafyumu na rangi Kisha koroga vizuri kuelekea upande mmoja
6. Weka dawa ya kuzuia kuharibika DM DMH Kisha koroga vizuri kabisa Kama unatumia chumvi weka kidogo kidogo huku ukipima uzito unaouhitaji Kisha koroga
7. Pima pH 5_7 Kisha iache ipoe baada ya saa moja Anza kufungasha shampoo yako
SHAMPOO YA TANGO
MAHITAJI /MALIGHAFI
VIFAA
Mzani, Ndoo Ya Plastiki, Gloves, Mask, Buti, Mwiko Wa Kukorogea
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chukua ndoo weka sless peke yake koroga mpaka owe cream
2. Weka maji kidogo kidogo mpaka yaishe huku ukiendelea kukoroga
3. Weka CDE na glycerine koroga kwa dakika tatu
4. Weka juisi ya tango Kisha koroga vizuri
5. Weka citric acid ,pafyumu na rangi Kisha koroga vizuri kuelekea upande mmoja
6. Weka dawa ya kuzuia kuharibika DM DMH Kisha koroga vizuri kabisa Kama unatumia chumvi weka kidogo kidogo huku ukipima uzito unaouhitaji Kisha koroga
7. Pima pH 5_7 Kisha iache ipoe baada ya saa moja Anza kufungasha shampoo yako
SHAMPOO YA ALOE VERA
Hii ni shampoo yenye virutubisho lishe vya aloe vera. Miongoni mwa vitamin zinazopatikana katika mmea huu ni vitamin B12 na B14 ambazo ni muhimu kwa ukuaji wa nywele. Hulainisha nywele kwa kuzuia ngozi kukauka, kuponya michubuko, kuzipatia nywele rangi yake na kuzuia nywele kujisokota.
MAHITAJI (LITA 10)
JINSI YA KUTENGENEZA.
1. Pima maji lita 10 kwa kutumia measuring cylinder na mimina kwenye chombo cha kuchanganyia
2. Chukua sless 1kg, gryceline 100ml, formaline 10ml, perfume 20ml na cde 200ml.Kisha vichanganye pembeni bila maji hadi vichanganyikane vizuri hadi sless iyeyuke kabisa.weka cmc/ alka 2 100gm kisha koroga tena vizuri hadi iyeyuke vizuri.
3. Weka juice yako ya aloe vera na koroga tena vizuri.
4. Malizia kwa kuweka rangi yako 10gm (kadiria) na weka DM DMH koroga tena hadi ishike vizuri.
5. Pima PH acha povu lishuke tayari kwa matumizi.
ANTI BACTERIAL HAND WASH/ SABUNI YA KUNAWIA
MAHITAJI
HATUA ZA UTENGENEZAJI
DAWA YA MADOA KWA NGUO ZA RANGI.
Mahitaji.
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
Utengenezaji
2. Tenga maji Lita 25 tia hypoclorite korogo iyeyuke yote, tia soda ash koroga dakika 10
3. Ongeza chumvi na hydrogen peroxide koroga vizuri funika acha kwa saa 24 kisha fungasha.
NB. Jaribu bidhaa yako kabla hujauza.
DAWA YA KUONDOA MADOA (jiki)
Malighafi
JINSI YA KUTENGENEZA
SHOWER GEL(sabuni ya kuogea )
Hii ni Sabuni ya maji ambayo iko maalumu kwa ajili ya kuogea
MAHITAJI
HATUA ZA UTENGENEZAJI
Mambo ya kuzingatia
Kama unaweka malighafi za mafuta ratio iwe 2% Hadi 5% sawa MLS 200 Hadi 600mls
WINDOW & GLASS CLEANER
Hii ni bidhaa ambayo hutumika kwa matumizi ya kusafishia vioo na vyombo mbalimbali aina ya glass. Huenda vioo vya madirisha au magari, watu wengi huwa wanamiliki vitu ambavyo vina material ya vioo na hawajui jinsi gani ya kusafisha hivyo vioo punde baada ya kuchafuka.
Hii ni bidhaa nzuri ambayo mara nyingi hutumika katika kusafishia madirisha ya vioo au kifaa chochote ambacho kimetengenezwa kwa material ya kioo,
MALIGHAFI ZITUMIKAZO KATIKA KUTENGENEZA
WINDOWS CLEANER
JINSI YA KITENGENEZA WINDOWS CLEANER
1. Utakuwa na maji lita kumi kama unataka kutengeneza lita kumi.Chukua sabuni yako lita moja kisha mimina katika chonbo chako ulicho aandaa ili utengeneze windows cleaner.
2. Chukua vinegar ( acetic gracial acid ) lita moja kisha uta mimina katikas chombo ambacho uliweka sabuni yako ya maji.. Kisha utakoroga mpaka utakapoona kuwa imekuwa vzuri kabisa. So povu litatokea jingi sana so unaweza ukaicha kwa kipindi flani hivi ( takribani dakika 5 ) mpaka utakapoona kuwa povu limetoka loteee.
Na hapo inakuwa umeweza kutengeneza windows cleaner kwa njia nyepesi kabisa.
SABUNI YA KUOSHEA MAGARI
Sabuni ya maji ya ya kuoshea magari ni moja ya sabuni pendwa sana mijini kutokana na urahisishaji wake ktk kuoshea magari pamoja na ubora wake.Sabuni ya maji ya kuoshea magari haipaswi kuwa na kemikali ili isipaushe magari na kupoteza ule mng'ao wa magari.Sabuni hii itaacha gari yako ktk mng'ao mzuri sana, pia haitapauka kutokana na malighafi hizi ambazo hazina kemikali.
Mahitaji:
KAZI ZA MALIGHAFI
HATUA ZA UTENGENEZAJI
Mtaji Tsh 24,000/= tu, sabuni Lita moja Tsh 3,000/=
AFTER SHAVE
MAHITAJI
UTENGENEZAJI
MATUMIZI: hutumika baada ya kunyoa(ku shave). mfano ukisha nyoa ndevu una paka hii after shave kuzuia kutokwa na vidonda au mapele.
MAFUTA YA MGANDO
Mafuta ya mgando ni mojawapo ya vilainishi vya ngozi vinavyoipa ngozi mwonekano wa kuvutia na nyororo.
Mahitaji.
Jinsi ya kutengeneza
NB: Mafuta haya yanaviwango vya TBS hivyo yafaa kwa matumizi ya watu wa rika na jinsia zote {Mtoto mdogo hadi mzee }
Mtaji wa mafuta ya mgando Lita 1.
Jumla Tsh 11,500/= tu
Utatoa mafuta 1000ml sawa na vichupa 20 vya 50ml kila kichupa uza Tsh 1,500 hadi 2000, vifaa kama Grycelin, rangi, pafyum, vitabaki.
MAFUTA YA KUREFUSHA NYWELE
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Yeyusha White Oil+Micro Wax kwa njia ya double boil.Ikiyeyuka weka Castrol Oil na uipue.
2. Chemsha Olive Oil Vijiko 6+Vitunguu swaumu+Vitunguu maji (Unaweza kusaga kabla) Kisha chuja na uchanganye kwenye mchanganyiko wa Awali.
3. Chukua tena Olive Oil Vijiko 5+Mvuje +Rosemary Chemsha Kisha uchuje na uchanganye kwenye mchanganyiko wa Awali.Koroga vyema.
4. Weka Rangi ya Mafuta (Kijani/njano hupendeza zaidi) Weka Perfume, koroga. Yakipoa mimina katika package ulizoziandaa yaache yagande Kisha tayari kwa matumizi.
MAFUTA YA MGANDO KWA RIKA ZOTE(WATOTO HADI WAZEE)
MAHITAJI
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
VIFAA
Jiko lenye moto, SufuriaIfungashio, Mwiko/kijiko cha kukorogea
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Washa jiko lako moto na ubandike sufuria.
2. Weka micro wax ndani ya sufuria na subiri iyeyuke,Kisha weka white oil lita 2 na koroga vizuri.Kisha ongeza coconut oil na Aloe vera gelly kisha koroga vizuri.
3. Weka Gryceline na uendelee kukoroga, weka perfume na koroga tena.Shusha mafuta yako na subiri yapoe (usiache yakapoa sana kwani yataganda kabla hujaweka kwenye vifungashio)
4. Weka kwenye vifungashio tayari kwa matumizi.
NB: Mafuta haya yanafaa kwa matumizi ya watu wa rika na jinsia zote.(watoto hadi wazee)
MAFUTA YA NAZI YA MGANDO
Mahitaji
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chukua sufuria weka jiko weka maji chukua nyingine ndogo kwa kutumia njia ya double boil,Weka vyote jikoni viyeyuke.
2. Vikishayeyuka na kuchanganyikana,ipua na uache yapoe.Yakishapoa mimina katika package ulizoziandaa yagande Kisha tayari kwa matumizi.
NB. Haya anaweza kutumia mtoto wa kuanzia miaka miwili na kuendelea.
UDI WA KUOGEA
UDI huu hutumika kuweka kwenye maji ya kuogea.Maji yanakuwa na harufu nzuri mno, badala ya kuweka hiriki, au mchaichai weka Udi unukie siku nzima.
MAHITAJI
JINSI YA KUTENGENEZA
NB: Kikopo huuzwa Tsh.1000 I nategemeana na eneo ulilopo.
UTENGENZAJI WA UBUYU WA VIPANDE
Mahitaji
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chemsha Maji jikoni weka sukari koroga mpakaiyeyuke kisha weka radha Na rangi koroga
2. Uache mkorogo wako uchemke had uanze kunata nata anza kuweka unga wa Ubuyu huku ukisonga kama ugali Na kuzidi kuongeza unga mpaka uishe
3. Ukisha changanyika vizuri anza kumimina kwenye chombo cha plastiki ulichoanza kupaka mafuta ya kula ili usigande ukikauka tandaza vizuri kisha uache ukauke
4. Ukikauka anza kukata vipande uvitakavyo wewe kwa ajili ya kuuza au kula
NB: weka maji zaidi ya robo lita kwa ajili ya akiba kama maji yatakuwa machache unaweka ya akiba hayo.
UBUYU
MAHITAJI
JINSI YA KUPIKA
1. Katika sufuria, weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki. Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri.
2. Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu. Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri. Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito. Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate Sana kiasi tu.
3. Kisha mimina ubuyu wa kokwa na changanya vizuri kabisa katika rojo. Endelea kupika vizuri kama dakika 2 hivi. Kisha mimina unga wa ubuyu na changanya vizuri tena.
4. Endelea kupika mpaka unaona sukari inaanza kuganda na kung'aa na kushika vizuri katika ubuyu.
5. Hapo sasa zima jiko na mimina ubuyu katika sinia kubwa na acha ubuyu upoe.
CHAKI
Chalk ni bidhaa ambayo imebuniwa kwa ajili ya matumizi ya shule, vyuo n.k
Chalk zinatofautiana kutokana na malighafi inayotumika, Rangi aina ya chokaa, Gypsum iliyotumika kutengenezea Isiyo na dust
(dustless)
CHALK No.1
Chalk ambayo malighafi yake ni CHOKAA.
Malighafi
Hii ni malighafi muhimu sana, na ndio malighafi kubwa inayotakiwa kwa kiwango kikubwa sana katika utengenezaji wa chaki hizo tunazozizungumzia. Kitaalamu au kisayansi zinaitwa “Calcium carbonate”. Hii inatengeneza uji mzito na kukauka kwa haraka sana pale inapochanganywa na maji. Mbali na kutengeneza chaki, inatumika hospitalini kutengenezea muhogo (Kiswahili cha mtaani) kuzunguka mguu au mkono uliovunjika
HATUA ZA KUTENGENEZA
1. Chokaa kilo moja na iwe imechekechwa na kupata unga ulio safi, Maji lita moja, Rangi ya chakula 10 mls.Mchanganyiko huu uchanganywe kwa pamoja na upate uji mzito, koroga kwa muda wa dakika 15.
2. Weka mchanganyiko wako katika mould ya fowl paper zikate ziwe na shape ya saizi ya chaki unayotaka ,Weka juani chaki zako mpaka zikauke Zikikauka, toa kwenye foil paper tuziingize jikoni kama tunavyochoma vyungu na matofali ili kuhahakikisha imeiva ukiishika inaacha vumbi mkononi na ikidondoka inakatika vipande vingi.
KANUNI ZA KUCHANGANYA CAUSTIC SODA NA MAJI KWA USAHIHI
KANUNI YA KWANZA
Kama Unatumia Hydrometer Unapima Baume 30
KANUNI YA PILI KWA VIPIMO VIDOGO 1.CAUSTIC SODA KILO MOJA MAJI LITA 3
CAUSTIC SOLUTION LITA MOJA MAFUTA LITA 2
Kwa kutumbukiza hyrometer kwenye caustic solution tupate baume 30 kama itakuwa imepungua ongeza
Caustic soda kisha koroga kupima tena kama imezidi ongeza maji kisha pima tena
NB: Vipimo hivi kwa wanaotumia hydrometer hata wale wasiotumia hydrometer wanatumia kutengeneza sabuni.
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
MOLD NA VIFYATULIO VYA SABUNI
- Kuna mold za aina nyingi zipo za chuma ambazo ukihitaji kumwagia mchanganyiko wako unapaka grisi.
- Kuna mold za mbao ambazo ziko ndogo kwa ajili sabuni za tiba za vipande pia zipo kubwa za sabuni ya mche au magadi
- Pia aina ya tatu kuna mold zinaitwa silicon mold kwa ajili ya sabuni za tiba za kuogea
Namna ya kudesign mold inategemea na vipimo vyako vya sabuni ambayo unataka iwe
Mfano mold ya sabuni za magadi urefu wa mche huo ndio uwe upana wa mold urefu na kimo unakadiria ila upana tu uwe unafanana na mche wa sabuni ambao ulionao kama sampo.
Mfano wa mold mbalimbali
SABUNI ZA MCHE/KIPANDE
MAHITAJI
Mfano wa sabuni ya mche
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Vaaa gloves chukua chombo Cha plastic weka mafuta na pia chukua ndoo weka caustic solution changanya na sodium silicate koroga ukimaliza
2. Chukua mchanganyiko wenye caustic solution + sodium' silicate nenda kaweke kidogo kidogo kwenye mafuta huku ukiendelea kukoroga weka rangi na pafyumu koroga
3. Kama unatumia mold ya chuma weka grisi kwenye mold au Kama unatumia mold ya mbao weka nailoni Anza kumwagia mchanganyiko wako na uache uakuke kwa masaaa kadhaa ukikauka Anza kukata tayari kwa kupelekea sokoni.
JEDWALI LA KANUNI
SABUNI ZA MAGADI (gwanji)
Ni moja ya sabuni ambazo zinapendwa Sana na kuweza kuteka soko kwa kiasi kikubwa sana.
MAHITAJI
Mfano wa sabuni ya Magadi
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1 Lita 5 Lita 2.5 Mls 50 5 gm
2 Lita 10 Lita 5 Mls 100 10 gm
3 Lita 20 Lita 10 Mls 200 20 gm
4 Lita 40 Lita 20 Mls 400 40 gm
1. CHUKUA NDOO YA PLASTIKI WEKA MAFUTA PIA
Chukua ndoo nyingine Pima caustic solution Lita 10 yenye BAUME 30
2. Chukua caustic solution weka sodium' silicate kuroga kwa muda wa dakika 2-3 ukimaliza Anza kumimikia mchanganyiko wa caustic solution na sodium silicate kwenye mafuta huku ukiwa unakoroga koroga kwa muda Hadi mchanganyiko uchanganyike vizuri
3. Chota uji wako kiasi Kama Lita mbili Hadi tatu weka pemben Pima rangi yako Anza kuchanganya na uji ule mdogo ulioutenga pembeni.
4. Chukia mchanganyiko wako mweupe Anza kumimina kwenye kibao Cha kufyatulia kidogo na Kisha unamimina wa rangi ya bluu kiasi unakuwa unafanya hivyo Hadi mchanganyiko wako wote uishe wa bluu na mweupe uki maliza chukua mti anza kuchoza zig zag au nane juu ya kibao Cha kufyatulia ukimaliza acha ukauke
5. Ukikauka Anza kukata sabuni yako kwa kufuata ukubwa ambao utakuwa unauhitaji
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
SABUNI ZA MAGADI
MAHITAJI
Jinsi ya kutengeneza
NB: Hifadhi uji wako sehemu yenye kivuli na uache wazi ili ugande.sabuni yako inakauka baada ya masaa 4 hadi 6 tayari kwa kukata.
BATIKI ZA AINA MBALIMBALI
Batiki ni nini?
Ni nguo au kitambaa cha pamba asilimia 100 kilichotiwa rangi kwa kuchora, kugonga, kuchovya, kunyunyiza au kuchubua.
Historia ya Batiki.
Batiki ilikua kama vazi lililoundwa au kubuniwa nchi za China na India, lakini kutokana na ukuaji na technolojia inavyozidi kukua ikasambaa mpaka kuingia hapa nchini kwetu na kushika hatamu. Hivi inavyokwenda wabunifu wengi wameweza kubuni kila aina ya mitindo mpaka kuipa sifa ya kuingia katika mitindo maalum ya Kitaifa.Ili iwe batiki lazima kuwe na aina fulani ya muundo bila hivyo itasomeka ni nguo ya kawaida tu.Batiki hutengenezwa kwa kutumia malighafi kadhaa.Malighafi hizi zote ni hatari na zinatakiwa kutumiwa na kutunzwa kwa uangalifu na mtu anaetumia basi lazima azijue hatari na jinsi ya kujilinda nazo. La sivyo anaweza kupata madhara makubwa na hatimae hata kupata vilema au matatizo ya kudumu au hata kifo.
AINA ZA BATIKI
BATIKI ZA KUCHOVYA (TIE AND DIE)
Ni aina ya nguo au vazi la asili linayotengenezwa kwa mikono kwa kuweka picha michoro na urembo mbalimbali.kwa hapa tanzania batiki soko lake kubwa na watu wengi wamejikita kufanya ujasiriamali huu unawaingizia kipato kikubwa na kuweza kumudu maisha yakitanzania
BATIKI ZA TIE AND DIE
Ni aina ya batiki ya kukunja mikunjo kwa kutumia mkono vilevile tie ni neon la kiingereza lenye maana ya funga na die ni neno la kiingereza lenye maana chovya hivyo basi ni batiki za kufunga mikunjo na kuchovya.
Malighafi
VITENDEA KAZI:
Meza, kitambaa cha pambe, kalamu, uzi, sindano, mkasi, kamba, sufuria kijiko kikubwa, ndoo au beseni, jiko, vibanio, maski na gloves.
AINA ZA TIE AND DYE.
Baadhi ya hizi zinaweza kuchanganywa na kupata rangi kama ifuatavyo Red +blue=purple yellow+blue =green yellow+orange=chungwa green+red=brown=udongo=green dark orange +blue=combat-rangi ya jeshi
JINSI YA KUTENGENEZA.
BATIKI ZA MISHUMAA
Mahitaji
VIFAA KINGA
- Gloves
- Miwani
- Viatu vigumu
- Brush
- Kiziba pua (barakoa)
- koti
Kazi za madawa
A. Sodium
B. Mshumaa
Kazi yake ni kuweka nembo ktk nguo na ktk vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo, twiga ,matunda au urembo wowote anaohitaji mtengenezaji.
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Weka mshumaa jikoni ili uweze kuyeyuka ukiyeyuka anza kukonga mshumaa kwenye kitambaa chako hakikisha unagonga mbalimbali kuruhusu kuweka mshumaa wa pili baada ya kuweka rangi ya kwanza acha mshumaa wako ukauke.
2. Uwekaji rangi,Chemsha maji ya moto yachemke sana Kisha pima Lita 3hadi 4 pima caustic vijiko 3, pima sodium vujiko 3 changanya na maji Moto tia rangi kijiko 2-3
Baada ya hapo pima maji lita 6 ya baridi Kisha changanya na mchanganyiko wa madawa awali kusudi yapoe yawe vuguvugu.
Tumbukiza vitambaa vinee vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuza geuza ili viingie rangi kwa dkk 20 Kisha suuza kwa maji ya baridi anika
3. Baada ya kukauka weka rangi ya kwanza chukua kitambaa chako chemsha mshumaa anza kugonga ua lingine kwenye kile kitambaa chemsha maji ongeza sodium hydrosulphate vijiko na rangi na caustic vijiko 3 koroga ongeza maji lita 5 anza kuchovya vitamba vyako viache kwa dakika 20 kisha suuza anika vikikauka nenda katoe mshumaa
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
Namna Ya Kutoa Mshumaa
Chemsha maji yachemke kabisa Kama ya kupikia ugali Kisha tumbukiza kimoja kimoja jikoni ili kuondoa mshumaa ktk kitambaa, Geuza kwa mti mrefu Kisha suuza kwa maji baridi anika kivulini na kabla hakijakauka vizuri piga pasi ili kuimarisha rangi.
BATIKI ZA KUBABUA / KUBLICH
Katika kutengeneza batiki za kubabua tunatumia kutengeneza kwa kutumia jiki na kumwagia kwenye kitambaa au kutumia sponji kuweka ua ambalounalihitaji
Mahitaji
JINSI YA UTENGENEZAJI
BATIKI ZA KUPRINT
Hizi ni batiki ambazo unatumia rangi na screen kwa ajili ya kutengeneza batiki hizi
Mahitaji
HATUA ZA UTENGENEZAJI
BATIKI YA KUPRINT
BATIKI ZA KUFINYANGA
Batiki hizi ni moja ya batiki rahisi kuliko zote hizi kwanza mchanganyiko wake unaandaliwa kama tie and dye za kuchovya.
MAHITAJI
HATUA ZA UTENGENEZAJI
SABUNI YA UNGA
MAHITAJI:
JINSI YA KUTENGENEZA:
NB: Rangi ya sabuni ya unga si sawa na rangi ya sabuni ya maji na ya sabuni ya maji si sawa na ile ya Sabuni ya mche
SIAGI YA KARANGA
MAHITAJI
NAMNA YA KUTAYARISHA
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
LOTION AND CREAM
Malighafi
KAZI ZA MALIGHAFI
HATUA ZA UTENGENEZAJI
Kumbuka
LOTION YA PARACHICHI
Lotion hii kwaajili ya kuifanya ngozi iwe ya asili( Natural soft skin).
Na haichubui hata kidogo.
MAHITAJI
UTENGENEZAJI
MATUMIZI:
LOTION YA LIMAO(LEMON
Lotion hii ni nzuri kwa wenye sura au ngozi yenye mafuta.Huondoa chunusi, mabaka na kuifanya ngozi yako ipendeze.
MAHITAJI
NB: PARAFFIN WAX - Unaweza kuongeza kama utahitaji lotion yako isiwe nzito.
UTENGENEZAJI
WHITENING & SOFTENING BODY SERUM
Hii ni kwaajili ya kung'arisha.
MAHITAJI
HATUA ZA UTENGENEZAJI
COFFEE BODY SCRUB (1kg )
Sasa hii ni jinsi ya kutengeneza coffee scrub bila kutumia sugar (sukari) endapo utataka kutengeneza emulsifying coffee sugar scrub maji hayahusiki. Hivyo hatutakuwa na kitu kinaitwa water phase.
MAHITAJI
Weka vyote kwenye sufuria ya stainless steel .
MAHITAJI
(Oil Phase)
Weka vyote kwenye sufuria ya pili kasoro (usiweke salicylic acid coffee powder potassium sorbate.
JINSI YA KUTENGENEZA.
Mpaka hapo Scrub itakuwa tayari, utaipack vizuri tayari kwa matumizi.
SUGAR SCRUB
(Mfano wa Pili wa Scrub)
MAHITAJI
Note: Sio lazima itumie butter nilizotumia na mafuta niliyotumia unaweka kuweka mengine kulingana na matakwa yako scrub isaidie nini kwenye ngozi.
UTENGENEZAJI
Pack kwenye vifungashio vyako tayari kwa matumizi au kupeleka sokoni.
SCRUB YENYE EXFOLIANT ZAIDI YA MOJA NATUMIA EXFOLLIANT ZAIDI YA MOJA . PIA SITATUMIA MAJI (SCRUB ITAKUWA EMULSIFYING )
EXFOLIANT NINAZOCHAGUA NI manjano na mchele. Nitahakikisha niko na fine powder zake
Mahitaji kutengeneza kilo moja ya scrub
UTENGENEZAJI
NATUMIA EXFOLLIANT ZAIDI YA MOJA PIA NITATUMIA MAJI SCRUB HII ITATAKUWA NA VIPENGELE VIWILI WATERPHASE NA OIL PHASE EXFOLLIANT
NILIZOCHAGUA KUTUMIA ni nyanya na tango Hakikisha una unga wa nyanya na tango MAHITAJI (kutengeneza kilo moja) waterphase (kipengele cha maji na malighafi zenye asili ya maji)
Weka vyote kwenye sufuria ya stainless steel kipengele cha pili oil phase mahitaji.
Weka vyote kwenye sufuria ya pili kasoro salicylic acid exfoliant zako ambazo ni tango na nyanya preservative yako ambayo ni potassium sorbate.
JINSI YA KUTENGENEZA
KAZI ZA BAADHI YA EXFOLIANT:
1. NYANYA - Hutumika kuondoa au kupunguza makunyanzi au mikunjo usoni au katika ngozi.
2. TANGO - Kuondoa chunusi na madoa.
TILES & SINK CLEANER
Malighafi
UTENGENEZAJI:
1. Weka sless katika ndoo yenye ujazo wa zaidi ya Lita 20 kisha koroga ongeza chumvi kidogo Kama gram 150 tu ili isaidie kuyeyusha sless kisha koroga vizuri Hadi kupata creamy na Kisha tia maji kidogo kidogo huku ukikoroga kuelekea upande mmoja, endelea kuongeza maji kidogo kidogo Hadi maji yaishe huku unakoroga.
Naamini makala hii itakuwa imekusaidia sana katika kujifunza mambo mbalimbali ambayo yataharakisha safari yako ya mafanikio. Ninakusihi ufanyie kazi yale uliyojifunza kwa bidii ili upate matokeo makubwa zaidi. Kumbuka kuwa una uwezo mkubwa sana ndani yako na kama ukiamua kuufanyia kazi basi hakuna kitu ambacho kitakuzuia. Nakutakia mafanikio katika ndoto yako na usisite kutembelea blog ya jumanne255.com kwa ajili ya kupata mafunzo mengi zaidi na pia endelea kuwasiliana nami kwa uhitaji wowote wa ushauri binafsi, mafunzo kwa wafanyakazi ama ushauri wa kibiashara.
KAMA UNATAKA KITABU CHA MAFUNZO CHA KUTENGENEZEA SABUNI N.K AMBAYO HAYAPO POPOTE UTAYAPATA KWENYE KITABU HIKI BONYEZA HAPA
Buy on
Tembelea Website hii: www.jumanne255.com (Utapata Makala nyingi za kujifunza/kukufundisha mambo mbalimbali)
Ni mkufunzi na mshauri katika Utengenezaji wa sabuni za aina zote, kwa ufanisi mkubwa kwenye vikundi mbalimbali ndani ya Tanzania na watu binafsi nafundisha.
0 Comments