Jumanne Mwita |
SUCCESS IS A PROCESS
Mimi ni kijana ambae bado kiumri ni mdogo pia muumini mkubwa sana wa HUSTLER, Huwa naamini katika kukua kidogo kidogo, Si muumini wa kulala Maskini na kuamka Tajiri. Naamini katika "Kidogo kidogo hujaza kibaba.
Namshukuru sana Mungu katika umri wangu mdogo nimeweza. Kupita mitihani mingi na migumu na yenye kunifunza, huwa nikikutana na kijana anapambana najihisi tuko wote katika tanuru hili ya Mapambano pia nashukuru nimeweza kupitia tanuru hili la ajira ingawa kuna muda utafika nitoke na kujiajiri, Kuna mengi nimeyaona kwenye ajira hizi tulizopo na nimejifunza mengi mno kwenye nyanja hizo na moja ya mambo makubwa niliyojifunza ni kuwa SUCCESS IS A PROCESS
Katika familia yetu sisi siwezi kusema ni familia Tajiri sisi ni moja ya familia masikini, kwani sisi ni zile familia ambazo.
Tulikuwa tunakula kutokana na tafuta yetu, Wazazi wangu hawakuwahi kuwa na biashara tofauti na kufanya vibarua popote itakapopatikana. Pamoja na hayo mlo wetu ulikuwa wakulenga na manati kesho tule keshokutwa tulale njaa.
Kwa kifupi walifanya vibarua kama wangekuwa wanashamba tukawa tunalima nafikiri maisha yetu yasingekuwa afadhali ya jana tungejikita kwenye Kilimo hata Ufugaji ili tule tushibe na nakumbuka kuna kipindi tuliwahi kulala njaa kama siku tano hivi kitu pekee kilichotusaidia ni unga uliobakia kama vibakuli viwili hivi tulikuwa tunapika uji mwepesi kabisa kwa mchana na usiku tu ili kupoza njaa.
Mama alijitahidi sana kupambana ili tusione maisha ni magumu na tusijue kama anaumia ila alipambana kama mwanaume jasiri hata kama hakuna chakula yeye alionyesha ni mtu ambae kesho anauhakika wa kupata na tukaishi.
Baba hakuwa mtu wa kujali sana matokeo yake alìkwenda kwa mdogo wake kuishi uko mapambano yakabaki kwa mama pamoja na kwamba alirudi ila bado hakuwa na msaada kwa wanae. Mama alihakikisha sikukuu tunavaa nguo mpya na shule tunaenda na kwa hilo alifanikiwa mama yetu sana.
Hakukuwa na maarifa ya kibiashara ambayo ningejifunza kwani nilikuwa bado ni mdogo, pamoja na udogo wangu nilikwenda kuomba omba kazi kwenye majumba ya watu ila sikufanikiwa kupata. Baadae niliamua kuokota Vyuma chakavu, ila mimi sikuwa kama watoto wa mtaani nilifanya kazi ya vyuma chakavu kama ajira kwangu maana ilinisaidia kununua mahitaji ya msingi pamoja na kumsaidia mama mahitaji yangu ya shuleni mama alinifunza zaidi ya kujiongeza na kunipa elimu juu ya pesa ninayoipata natakiwa kuifanyia kitu gani ili niweze kujipambania mimi kama mimi elimu hiyo haikuishia kwangu tu bali hata kwa kaka yangu pia alimwambia.
Baadae nikiwa darasa la 3 kwenda darasa la 4 nilianza kuuza, Miwa na maembe. Nilifanya hivi kwa mtaji kidogo nilioupata baada ya kwenda kulima vibarua nikalipwa senti chache, niliumia kufanya kazi kubwa na kulipwa kidogo pia sikukata tamaa pesa zile sikuzitumia vibaya bali nilitunza zinisaidie baadae, haikutosha nikaenda kufanya vibarua vya ujenzi kama saidia fundi nikatunza kisha nikanunua mahitaji ya shule.
Katika maisha yangu nilipenda sana siku moja niwe Mfugaji ila sikufanikiwa mpaka sasa, nilijaribu kwa pesa niliyoipata nilinunua kuku na bata nikawafuga nikijua watanisaidia, Baadae nikapata wazo nikanunua na njiwa nikawa nawafuga baadae njiwa nao pia walikuwa kamradi kangu. Njiwa zikaliwa na paka zingine zikakimbia sijui ziliko ishia.
Unajua ilikuwa mwaka gani huo? Ni miaka ya 2004s huko sijui wewe ulikuwa wapi mtu wangu.
Sasa baada ya harakati zote hizo. Maisha yalisonga, hapakuwa na utajiri, hapakuwa na mafanikio ya kifedha ila palikuwa na mafanikio ya kiakili niliweza kujifunza mengi bila kushikiwa fimbo ilinisaidia kujua thamani ya fedha.
Umri ukasonga maisha yakaendelea kwenye harakati zangu mwisho nikapata kazi kwenye Taasisi binafsi ya fedha nikaenda nikaonana na bosi mwenyewe tukaelewana bei ya malipo kila mwezi kazi ikaendelea hapo sasa nimeajiriwa 2013s,
Nikagundua kumbe mjini ni akili, hata ajira tunazopewa tukalipwa mamilioni bado ni mtego kamwe huwezi kuendelea kwa huo mshahara labda uwe mwizi na ukweli ni kuwa watumishi wengi ni wezi. Sababu tayari muda wako umeuuza kwa mwajiri wako bila kulazimishwa... Anyway tuyaache hayo.
Sasa kwenye hizi harakati zote nakuhakikishia pesa yangu kubwa ambayo nimewahi kuwa nayo kwa wakati mmoja haizidi milioni moja hata kama itazidi ni kidogo sana ila sidhani kama nimewahi kuwa na milioni 2.
Baadae tunarudi palepale kwenye mfumo wangu wa maisha wa kuamini katika HUSTLE, Licha ya kuwa sijawahi. Kuwa na Milioni hata 10 lakini kwa umri wangu mdogo sana nimefanikiwa sana kupitia hiyo slow slow. Na ndio maana nashauri sana watu waache kuamini kuwa maisha tunaweza kuyabahatisha mafanikio. Mimi kuna wakati naibiwa, natapeliwa, nadhulumiwa na kukatishwa tamaa sana.
Ila haijawahi kuwa sababu ya kuamini katika shortcut. Sijawahi kuona kama nachelewa kwa lolote ilimradi napumua.
Nawekeza kwa watu kama sina pesa na hilo linanilipa sana. Naishi maisha yangu kwa sasa naweza simlipi mtu kodi kwenye nyumba ninayoishi,
Kitu pekee ninachotaka kukikwepa na kabla ya miaka 2 ijayo ni kumsujudia mtu ili nipate kushiba. Haya yote sio kwamba nitayafanikisha kwa huruma bari kwa Hustle zangu ndio zitanivusha hapa. Nimejitoa sana, Kuanzia mwaka 2003 mpaka leo sijawahi kujiona kama nimekosa chochote licha ya kuwa sijawahi kuwa na chochote.
Huwa naamini katika kufanya kile Ninachoweza kisha namkabidhi Mungu.
Mshahara au malipo hayajawahi kuwa kipimo cha juhudi zangu katika kufanya chochote.
Mimi nikifanya kitu nakifanya kwa juhudi zangu zote na kwa nia njema, hata nikijua mwisho hautanilipa bado nitaongeza juhudi. Huku mijini tunakutana na watu wengi wa kila aina Wenye navyo na wasiokuwa navyo. Sijawahi kujiskia mnyonge kisa fulani anacho mimi sina. Huwa namshukuru sana Mungu kwa kila kitu.
Simdharau mtu sababu ya hali yake yoyote na naamini kila mtu ana mchango wake kwenye hatua zangu.
Hata kwenye hii mitandao ambapo wengi hatujuani bado nimekuwa nikijaribu kumwangalia kila mtu kwa jicho la faida, hata kama hatupeani shekeli ila tunakuzana bongo zetu.
Niendelee kukumbusha kuwa ikiwa tunataka mafanikio lazima tukubali kuwa na TABIA CHANYA Tabia hizi tunatakiwa kuwa nazo hata tukiwa hatuna kitu, Mafanikio siyo suala la kuhamisha bali ni mchakato na kama hatujapata pesa basi angalau mafanikio yetu yaanzie kichwani.
Bongo zetu ziwe zinachaji, ziwachajishe na Wengine.
UMASKINI SIYO SIFA.
1 Comments
Hunger bro na Pole sana kwa mikasa ya maisha
ReplyDelete