NEW

6/recent/ticker-posts

Advertisement

Je Unafahamu kifurushi cha Bima "Afya Salama Health Plan" kutoka Kampuni ya Strategis Insurance (T) Limited?

Habari wana Blogger,

Juzi nilikuwa kwenye jukwaa la JF nikauliza kuhusu kampuni za bima ambazo zinatoa huduma bora na gharama nafuu za bima ya afya nchini Tanzania. Baada ya majadiliano mengi, nikaamua kwenda hospitali moja ya mzungu huko Bukombe District Council, mtaa wa Maganzo, kuulizia bima wanazopokea. 

Reception walinipa muongozo, na moja ya bima walizopendekeza ni Strategis Insurance (T) Limited, inayotoa kifurushi cha Afya Salama Health Plan. Kifurushi hiki kinahusu familia kuanzia watu wanne, na ukiwa na zaidi ya wanne, inabidi ulipie zaidi.

Niliamua kuendelea kuuliza maswali ili nijue zaidi kuhusu bima hii na kuhakikisha siangukiwe na promo isiyo na msaada.

Nilichotaka kujua ni je, bima hii inaruhusu kulazwa? Walijibu ndio, lakini kuna huduma ambazo hazipatikani kupitia bima hii, zikiwemo:

HUDUMA AMBAZO HAZIPO KATIKA BIMA HII:

  • Gharama zilizokwisha lipwa na bima nyingine kwa tatizo/ugonjwa huo huo
  • Magonjwa au matatizo ya meno na macho isipokuwa yale yanayotokana na ajali
  • Matibabu yaliyofanyika kwa mtoa huduma asiyekuwa na mkataba na Strategis Insurance (T) Limited
  • Matibabu au upasuaji wa urembo ama upasuaji wa plastiki
  • Uzazi wa mpango na matibabu ya utasa
  • Matibabu ya mwanachama kulipa fedha taslimu kwa mtoa huduma kwa lengo la kuomba kurudishiwa fedha

Pia niliuliza sifa za mtu anayehitaji kujiunga na bima hii, na walinijibu kuwa:

SIFA ZA ANAYESTAHILI KUJIUNGA NA MPANGO HUU WA BIMA:

  • Umri wa juu wa kujiunga ni miaka 70
  • Ukubwa wa familia ni mwanachama na wategemezi watano, ikijumuisha mwenza wa ndoa na watoto wanne wenye umri chini ya miaka 18. Pia, mtoto tegemezi mwenye umri chini ya miaka 21 ambaye hajaoa/kuolewa na bado ni mwanafunzi.
  • Mwanachama ataruhusiwa kupata huduma kupitia vituo vya afya, hospitali, na maduka ya dawa yaliyoorodheshwa.

KIPINDI CHA KUSUBIRIA:

  • Miezi tisa ya kusubiria kwa matibabu yote yanayohusiana na uzazi
  • Miezi kumi na mbili ya kusubiria kwa matibabu ya kulazwa ya muda mrefu na magonjwa yaliyokuwepo kabla ya kujiunga na bima

MALIPO YA MWAKA YA BIMA KWA FAMILIA:

  • TZS 200,000 kwa mwanachama pekee hadi familia ya watu wanne (M+3). Ukiwa na zaidi ya wanne, inabidi ulipie TZS 80,000 zaidi kwa kila mtu kwa mwaka, jumla TZS 280,000.

Bima hii inatolewa na wakala wao NMB Bank PLC. Unaweza kupata fomu zao kwenye tawi lolote la NMB kwa kuulizia huduma ya Strategis Insurance Afya Salama Health Plan.

Nawaomba wale ambao wanatumia huduma za Strategis Insurance watupatie mawazo na uzoefu wao ili tuweze kusaidiana katika kuhakikisha familia zetu zinakuwa na furaha na afya njema.

Asante sana kwa kusoma na karibu kwenye mjadala.

Post a Comment

0 Comments