NEW

6/recent/ticker-posts

Advertisement

Video ya Gesi Asilia Inayovuja Kisima cha Maji Yasambaa: Serikali Yatakiwa Kuchukua Hatua za Haraka na Kufuatilia Ukamilifu wa Rasilimali za Taifa



Waheshimiwa: Waziri wa Madini, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan


Napenda kuwasilisha taarifa hii ya video inayosambaa mitandaoni, ikionesha gesi asilia inayovuja kupitia kizima cha maji. Video hii ni ishara ya jambo kubwa, na ni muhimu kama viongozi wenye dhamana mfanye uchunguzi wa haraka kujua ukweli wake. Je, gesi hii ipo wapi? Na kama ni video ya zamani, basi tunahitaji kujua hatua gani zilichukuliwa?

Tunawakumbusha kuwa tumeshaona mfano wa ugunduzi wa madini ya Tanzanite, ambapo wananchi wa kawaida waligundua madini haya lakini hawakufaidika, huku madini yakiuzwa kwa bei ndogo na kuondoka yote. Tunahofia kwamba huenda gesi hii pia ikawa hadithi nyingine ya kupoteza fursa kwa taifa letu. Je, tutairudia historia kama ilivyotokea na gesi ya Mtwara au madini mengine?


Kwa kuwa video hii imeonekana na wengi, inahitajika ifanyiwe uchunguzi wa kina. Kama viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali za nchi hii, tunaomba hatua za haraka zichukuliwe ili kuhakikisha kuwa rasilimali hizi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote, na si vinginevyo.

Tunaomba utaratibu wa wazi kuhusu hali halisi ya gesi hii na hatua zinazochukuliwa na serikali kufuatilia suala hili.

Post a Comment

0 Comments